BBC

Mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini Guinea yanasema yanaamini zaidi ya mashabiki 135 wa kandanda walifariki katika mkanyagano katika uwanja wa mpira siku ya Jumapili, wengi wao wakiwa watoto.

Idadi hiyo, ambayo haijathibitishwa, ni kubwa kuliko idadi rasmi ya vifo ambayo ni watu 56.

Makundi hayo yanasema makadirio hayo yanatokana na taarifa kutoka hospitali, makaburi, mashahidi katika uwanja huo, familia za wahanga, misikiti, makanisa na vyombo vya habari vya ndani. Watu wengine 50 bado hawajulikani walipo, ilisema.

Hata hivyo, serikali ya kijeshi, imeonya dhidi ya kueneza habari “ambazo hazijathibitishwa,” ikisema uchunguzi wake unaendelea kuhusu mkasa huo katika mji wa pili kwa ukubwa nchini humo, Nzérékoré.

Tukio hilo baya lilitokea baada ya uamuzi wa kutatanisha wa mwamuzi wakati wa mechi, ambao ulisababisha vurugu. Polisi walijibu kwa kurusha mabomu ya machozi, wakati watu wakijaribu kukimbia.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema kulikuwa na matumizi ya kupindukia ya gesi ya kutoa machozi katika eneo dogo, na kuongeza kuwa magari yaliyokuwa yamewabeba maafisa waliokuwa wakitoka uwanjani pia yaliwagonga raia waliokuwa wakijaribu kutoroka.

Waziri Mkuu Mamadou Oury Bah Jumanne alitangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kwa waathiriwa.

Guinea ni miongoni mwa nchi kadhaa za Afrika ambazo kwa sasa zimepigwa marufuku kufanya mechi za kimataifa za soka kwa kutokidhi viwango vya kimataifa.

Nchi nyingine zilizozuiliwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kufanya mechi za kimataifa ni pamoja na Ethiopia, Gambia, Chad na Sierra Leon

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *