
Mahakama imekataa ombi la kuwaita Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, pamoja na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa kutoa ushahidi katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu.
Mahakama imeeleza kuwa si sahihi kuwaita mashahidi hao kwa madhumuni ya kuthibitisha iwapo walitishika au hawakutishika kutokana na kauli zinazolalamikiwa katika shauri hilo.
“Kuhusu mashahidi wengine, mtakumbuka kwamba tarehe 21 Agosti Mahakama hii ilitoa uamuzi mdogo kwamba mshtakiwa ana kesi ya kujibu na ikamweleza kuwa ana haki ya kuleta mashahidi wake,” Mahakama imesema.
Katika orodha ya mashahidi aliowataja, walikuwemo:
- Samia Suluhu Hassan
- Dk. Philip Mpango
- Kassim Majaliwa
- Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP)
- Jenerali John Jacob Mkunda, Mkuu wa Majeshi
- Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa
- Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Ramadhani Kingai
- Wengine ni John Mnyika, Amani Golugwa, John Heche na Brenda.
“Baada ya kuwasilisha orodha hiyo, mshtakiwa aliiomba Mahakama itoe wito kwa mashahidi hao ili waweze kufika kutoa Ushahidi,” Mahakama iliendelea kusema.