Meneja wa duka la bidhaa za plastiki ambaye ni raia wa kigeni kutoka China Bw. Wang Zhan, anadaiwa kwenda kinyume na sheria mbalimbali za nchi.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari cha kuaminika Bw. Wang anadaiwa kukiuka sheria ya ajira kwa kutowatendea haki wafanyakazi wake.

Chanzo cha habari kimeiambia Morningstar post hivi karibuni kuwa Meneja huyo Bw. Wang, amekuwa hatoi mikataba ya ajira kwa baadhi ya wafanyakazi wake.

Pia, anadaiwa kuwa hawaandikishi wafanyakazi wake kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii hivyo kuwanyima haki zao za ajira, pia wanafanya kazi siku za jumapili na sikukuu bila ya malipo ya ziada,

Morningstar post ilimtafuta Bw. Wang ofisini kwake barabara ya Kongo ili kufafanua taarifa hizi, lakini alikwepa kuzungumza na waandishi wa habari .

Bw. Wang alimpa nafasi mkalimani wake ambaye naye pia aligeuka bubu akikataa kata kata kuzungumza na wanahabari.

Hata hivyo, juhudi za kutafuta ufafanuzi wa taarifa hizi kwenye mamlaka husika zinaendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *