Na Mwandishi Wetu, Nanyumbu

Viongozi wa serikali ya Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara, wameweza kutekeleza agizo la serikali la kuuza sukari kwa bei elekezi katika wilaya hiyo.

Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na tovuti hii, umebaini kuwa sukari katika wilaya ya Nanyumbu kwa sehemu kubwa inauzwa kwa bei elekezi iliyoagizwa na serikali.

Serikali kupitia kwa Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari Nchini (SBT),  Profesa Keneth Bengesi, ilitoa agizo la ukomo wa kuuza sukari kwa bei elekezi nchini ya sh 3200.

Agizo hilo la serikali limekuwa likisuasua katika baadhi ya maeneo nchini na hivyo sukari kuadimika na sehemu zingine inauzwa kwa bei ya juu tofauti na bei elekezi ya serikali.

Morningstar Post, ilizungumza na baadhi ya wafanyabiashara katika wilaya ya Nanyumbu wanasema kuwa wanatii amri ya serikali.

“Hatuwezi kuacha kutii agizo la serikali ndio maana unaona watu wengi wanauza kwa kufuata bei elekezi ya serikali” Alisema Musa Rajabu.

Musa anasema kuwa bei ya sukari iliyotolewa na serikali ni elekezi hivyo hakuna mfanyabiashra ambaye anaweza kupinga agizo la serikali.

Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu, Dkt Stephen Mwakajumilo akizungumza na Morningstar Post alisema kuwa katika wilaya yake ametoa maagizo kwa watendaji wote kuhakikisha sukari inauzwa kwa bei ilekezi iliyotolewa na serikai na mfanyabishara anayekiuka agizo hilo hatua kali huchukuliwa dhidi yake.

Alisema kuwa wameweza kufanya hivyo kwa kuhakikisha watendaji wa halmashauri wanafanya  ukaguzi mara kwa mara kuhakikisha kuwa agizo la serikali la kuuzwa kwa sukari kwa bei elekezi ya sh 3200 linatekelezwa.

Alisema kuwa mbali na agizo hilo wafanyabiashara wameitikia wito na wengi wamekuwa waaminifu kutii agizo la serikali.

Licha wafanyabiashara wa Nanyumbu kutii amri ya serikali  baadhi ya maeneo ya jijini Dar es Salaam, wafanyabiashara wameanza kupunguza bei lakini hawafuati bei elekezi.

Bei ya sukari katika baadhi ya  maeneo ya Dar es Salaam sukari imetoka kuuzwa sh5000 na baadhi ya maeneo imepungua hadi sh4000.

Uchunguzi wa Morningstar inaonesha kuwa bado wafanyabiashara wameendelea kuficha sukuri na hivyo sukari kuadimika kwenye baadhi ya maeneo nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *