28 Februari 2024
Beki wa Liverpool na Scotland Andy Robertson, 29, ndiye mlengwa mkuu wa mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wakati wakipanga jinsi ya kujaza nafasi ya mchezaji wa kimataifa wa Canada Alphonso Davies, ambaye anaonekana yuko tayari kujiunga na Real Madrid. (Daily Mail)
Wasiwasi wa Arsenal juu ya kiwango cha majeruhi ya mshambuliaji wa Brazil Gabriel Jesus ni sababu kubwa ya kutafuta mshambuliaji wao, huku Ivan Toney wa Brentford, Victor Osimhen wa Napoli, Joshua Zirkzee wa Bologna na Viktor Gyokeres wa Sporting wakiwa miongoni mwa wachezaji wanaolengwa. (Daily Mail)
The Gunners wanamtaka beki wa Ajax Jorrel Hato, 17, lakini klabu hiyo ya Uholanzi ina matumaini ya kumshawishi asaini mkataba mpya. (Evening Standard)