
Lissu: Nasema hivyo kwa sababu uchaguzi unafanyika kwa mujibu wa sheria na katiba. Serikali ndiyo inayosimamia sheria, iliitisha serikali kwa kuikata sheria ambayo imewekwa, kuikaidi sheria iliyowekwa na serikali ni kosa.
Hapa ndipo kesi hii ipo, mtakumbuka kwamba PW1 alikiri kwamba kwenye hayo wanayolalamikia hakuna neno serikali wala hakuna neno Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wala hakuna neno Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, wala hakuna maneno rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , wala hakuna maneno Makamu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wala hakuna maneno Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na zaidi ya hapo hakuna Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam na kwa maneno yake ukurasa wa 157.
Hivyo hicho wanachodai kimetishiwa hakipo. Serikali yenyewe haipo na jina la kiongozi yeyote wa kiserikali lililotajwa huko ni kukiri kwake kwenye maswali ya dodoso.
Licha ya hayo PW1 aliendelea kusisitiza kuwa serikali ilipangwa kutishiwa akasema “mtu anaposema ‘kukinukisha sana’ umetenda uhaini, maneno kukinukisha sana, kukinukisha vibaya sana, hayapo kwenye sheria isipokuwa ukiyasema umefanya kosa la uhaini kwa sababu serikali ndiyo inayosimamia sheria kwa hiyo unakuwa umetenda uhaini” huo ndiyo ushahidi unawashawishi mtoe hukumu ya kunyonga mtu…hawana hata aibu.
Lissu: Ushahidi ulipo kwenye ushahidi wa PW1 kusema huu ni uhaini ukawa wimbo wa mapolisi wote na mawakili wote wa serikali waliopo mbele yenu…alipoamua tu kwamba huu ni uhaini hakuna kitu chochote kingebadili mawazo yake.
Alipoulizwa PW17 aliyekuwa shahidi wa kuona na kusikia kwenye mkutano wala hakuona shida yoyote alipoambiwa hivyo alisema “ni kweli.
Kwenye maelezo yake PW17 alisema ”mlikuwa mnazungumzia changamoto zinazowakabili na pia mlikuwa mnazungumzia sera yenu ya no reform no election nimesoma maelezo yake na nikaamua kufungua kesi ya uhaini ni mimi ndiye niliyeamua kufungua faili la uhaini”.
Baada ya kusoma maelezo yote” D16 ni maelezo ya PW17 ambayo PW1 anakiri anayasoma hayajasema kulikuwa na kosa lolote achilia mbali suala la uhaini, hivyo hakuna ambacho kingembadilisha.
Alipoulizwa na mawakili wa serikali. Unasema juu ya hayo maneno yanaweza kuihusu serikali ya Jamhuri ya Muungano?
Kumbuka amesema maneno serikali ya Jamhuri ya Muungano hayapo, je hayo maneno yakibaki yanaweza kuihusu serikali pia alisema “Hayo maneno yaliyonukuliwa kwenye maelezo yake kwa muktadha wake yanamaanisha serikali”.
Akaendelea kurudia maneno kwa vile uchgauzi unafanyika kwa sheria na katiba hivyo hayo maneno serikali yapo kwenye maneno ambayo tunalalamikia hayapo lakini yapo”.
Kisichokuwepo kinaingizwa huo ni ushahidi wa PW1 alipotoa ushahidi huohuo ndiyo ukawa msimamo wa kila polisi aliyekuja hapa kutoa ushahidi, yeye ndiye aliyewaweka polisi waseme nini kila polisi ushahidi wao unafanana kama sare wanazo vaa.