MGODI WA DHAHABU WAVAMIWA RUANGWA

Waswahili walisema ‘penye riziki hapakosi fitina’ .

Wachimbaji wadogo wadogo wa dhababu mgodi wa Kambenga Kijiji cha Mbekenyela Wilaya ya Lindi, wameingia kwenye mgogoro na baadhi ya mafisa wa ngazi za juu wa Jeshi la Wananchi nchini (JWTZ).

Wachimbaji hao wameingia katika mgogoro baada ya kuwakaribisha baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa wanajeshi wa ngazi za juu wa jeshi nchini ili kufanya shughuli za uchimbaji kwa pamoja.

Wakiongea na Morningstar post kwa njia ya simu kwa sharti la kutotaja majina yao, walisema awali waligundua maeneo ambayo dhahabu inapatikana kirahisi na walianza kuchimba bila ya vibali kutoka stamico mkoa Lindi.

Walisema walianza kuchumba mgodi huo bila vibali na walikuwa wanatumia vifaa duni, lakini walikuwa wanapata dhahabu kidogo bila kusumbuliwa na mtu yeyote.

Wakaongeza kuwa baada ya kuwakaribisha maofisa hao (majina tunayo) walileta vifaa vya kisasa vya kuchimba ili kuboresha utendaji kazi.

Walisena walikubaliana na matajiri hao kushirikiana kuchimba dhahabu na kugawana faida baada ya kutoa hela za matumizi .lakini ghafla baada ya kuanza kupata dhahabu nyingi kuliko awali iliandaliwa mikataba ambayo ilionekana kama wao ni wafanyakazi wa hao matajiri ndipo ilibidi waende kwa afisa madini mkazi mkoa wa Lindi injinia Emmanuel shija ili asuluhishe mgogoro huo.

Walisema baada ya kikao na afisa madini ambacho kiilichochukua wawakilishi 15 kila upande, afisa madini alifunga mgodi kwa kuwa wote hawakua na leseni.

Uchunguzi uliofanywa na Morningstar post umebaini amri ya kuacha kuchimba dhahabu kwenye mgodi huo ilishindwa kutekelezwa kwa sababu baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Lindi na baadhi ya viongozi wa serikali wananufaika na uvamizi huo wakiwemo baadhi maafisa polisi..

Uchunguzi umebaini pia kuwa eneo hilo ni la kampuni ya Jitegemee iliwahi kupewa leseni ya utafiti wa madini katika eneo hilo.

Morningstar POST ilimtafuta afisa madini mkoa Lindi kutaka kujua mgogoro huu injinia Shija alikiri kuwepo kwa mgogoro huo lakini niliutatua alijibu injinia Shija kwa njia ya simu na pia alipoulizwa kuwa amri yake ya kufunga mgodi haikutekelezwa alisema hajui kama mgodi huu unaendelea na ameahidi kufuatilia na kuchukua hatua akibaini unaendelea

Aidha Oktoba 2 mwaka huo vijana watano walikamatwa na polisi wilayani Ruangwa kwa kudaiwa kukutwa na mabaki ya unga wa dhahabu kwenye glofsi na kupata dhamana jana kitendo kilicholalamikiwa na washirika wa mgodi huo
Pia Morningstar imemtafuta Kamanda wa Polisi wa mkoa Lindi kujua hatua zitakazofuata baada watuhumiwa kupata dhamana, tutaendelea kufuatilia sakata hili na kuwajuza wasomaji wetu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *