Na Mwandishi Wetu

Diwani wa kata ya Azimio, Temeke jijini Dar es Salaam, Bi. Amin Lalani, ameahidi kumchukulia hatua kali mfanyabiashara mmoja katika kata hiyo anayefahamika kwa jina la Zomboko.

Diwani huyo amesema atakwenda kutembelea yadi ya mfanyabiashara huyo anayedaiwa kuwa anauza mafuta ya petrol na disel kiholela bila kuwa na vibali katika yadi yake iliyoko kwenye makazi ya watu.

Akizungumza na Morningstar Post, Mheshimiwa diwani Bi Amina, alisema kuwa aliwahi kupita kwenye yadi ya mfanyabiashara huyo na kukuta gari la polisi likiwa limepaki, lakini hakujua nini kilikuwa kinaendelea.

Alisema kuwa anamfahamu mfanyabiashara huyo kuwa ana magari ya kusafirisha mafuta, lakini taarifa za kuuza mafuta bila vibali hana uhakika nazo, lakini ana wasiwasi huenda biashara hiyo itakuwa inafanyika kwa sababu aliwahi kukuta polisi wakiwa wamebaki kwenye yadi hiyo wakizungumza na watu wa yadi hiyo.

“Sina uhakika lakini kuna siku niliwahi kupita pale nikakuta gari ya polisi ikiwa imepaki, wakizungumza nao, inawezekana kinachozungumzwa ni kweli, kesho ntakwenda pale na kama ntakuta hali yoyote ntawapigia simu (waandishi), ” alisema Mheshimiwa diwani alipokuwa akizungumza na Morningstar Post kwa njia ya simu.

Mheshimiwa diwani alitoa ufafanuzi huo baada ya waandishi wa habari wa Morningstar Post kutaka kuthibitisha kama anamfahamu mfanyabiashra huyo katika kata yake na biashara anazofanya.

Akizungumza na Morningstar Post kwa njia ya simu mfanyabiashara huyo maarufu kwa jina la Zomboko, alisema kuwa yeye ni mfanyabishara wa magari ya kusafirisha mafuta taarifa kuwa anauza mafuta ya “videbe” sio za kweli.

Hata hivyo baada ya kuthibitishiwa na waandishi wa habari hizi kuwa kuna baadhi ya picha zilizopigwa kwenye yadi yake alitaka kuonana na waandisihi wa habari hizi ofisini kwake ili wamuoneshe picha hizo.

Hata hivyo alipotafutwa na waandishi ofisini kwake hakuweza kupatikana kuzungumzia zaidi taarifa hizo, na alipopigiwa simu alisema kuwa yuko nje ya ofisi.

Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Morningstar Post, Bw. Zomboko anadaiwa amekuwa akinunua mafuta kihole kutoka wa watumishi wa serikali wasio waaminifu na wale wa kwenye mradi wa SGR na kuuza mafuta hayo kiholela kwenye yadi yake.

Baadhi ya maaskari na maafisa wa TRA mara kadhaa wamekuwa wakimkamata lakini biashara hiyo inadaiwa kuendelea.

Morningstara inaendelea kufuatilia zaidi kwa viongozi wa kata na polisi kuzungumzia suala hili.

0744 499 499

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *