Na Mwandishi Wetu
Wakazi wa Masaki Kata ya Msasani jijini Dar es Salaam, wameeleza kufurahishwa kwao na kuhamishwa kwa Katibu Tawala wa Wilaya (DAS) kutoka jijini Dar es Salaam.
Wakazi hao wametoa hisia zao baada ya uteuzi mpya wa kuwahamisha DAS uliofanywa hivi karibuni.
Hatua hiyo imewafurahisha wakazi hao wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi hao ambao hawakupenda kutajwa majina yao, walisema DAS huyo ambaye jina lake tunalihifadhi aliyekuwa akiishi katika maeneo hayo amekuwa akionesha dharau kubwa kwa majirani zake pamoja na uongozi wa serikali ya mtaa huo.
Waliongeza kuwa DAS huyo ambaye inadaiwa kuwa ameoa mtoto wa kigogo serikalini, amekuwa hazungumzi vizuri na wafanyabishara wa mtaani kwake pamoja na majirani wenzake na kunapokuwa na vikao vya pamoja kutatua changamoto za mtaani kwake huwa haudhulii vikao hivyo.
Pia, wanasema kuwa wakati mwingine amekuwa akisigana na wafanayabiashara mtaani kwake hasa wale wanaouza vinywaji kwenye ‘grocery’ na baa akihisi kwamba wanampigia kelele.
DAS huyo amekuwa akijigamba kwa uwezo wa fedha na nafasi yake ya kazi na kwa kuwa mkewe anamahusiano na kigogo mzito wa serikali.
