Na Emmanuel Lyimo

Mabasi ya Mwendokasi ya jijini Dar es Salaam, DART yamekuwa yakisababisha usumbufu mkubwa kwa abiria wanaotumia mabasi hayo katika jiji hilo.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa Morningstar POST, umeonesha kuwa mabasi hayo yamekuwa yakifanya kazi bila kuwa na utaratibu unaoeleweka.

Mabasi yamekuwa yakichelewa kufika kwenye vituo na  kusababisha msongamano mkubwa wa abiria vituoni haswa wakati wa jiioni na asubuhi kusababisha abiria kugombania na kusababisha wizi kwa abiria kuibiwa mifukoni.

Mabasi yamekuwa yakiegeshwa kwenye vituo badala ya kufanya kazi wakati abiria wakiwa wamejazana vituoni madereva wa mabasi hayo wanaengesha magari na kuzungumza na simu.

Aidha huduma ya mabasi ya mwendokasi imekuwa kero kwa abiria kwani wauzaji wa tiketi wamekuwa wakileta usumbufu kwa abiria wanaokata tiketi kwa kudai kuwa hawana chenji na kusbabisha msongamano mkubwa wa watu vituoni abiria wakikaa kwenye msululu wa foleni kusubiri chenji.

Uchunguzi uliofanywa kwenye kituo cha mabasi ya mwendokasi cha Kimara mwisho madirisha ya kuuza tiketi mengi lakini wakati mwingine linafunguliwa dirisha moja tu na kusababisha msululu wa watu kwenye foleni bila sababu.

Akizungumza na Morningstar POST , abiria mmoja mkazi wa Kimara, Jofrey Yakob alisema kuwa baadhi ya wafanyakazi wa mabasi ya mwendokasi asilimia kubwa wamekuwa hawana nidhamu kwa abiria kwa kutuma lugha chafu kwa abiria.

“Wafanyakazi hawa wamekuwa wakitusumbua sana ukiwauliza wanakujibu kijeuri wengine hawana habari ya kuelekeza abiria” alisema Jofrey.

Akizungumzia mabasi hayo Jofrey alisema kuwa mabasi haya yanafanya usumbufu kwa abiri kutokana kuwa hakuna mshindani katika biashara hii ni bora serikali ilete washindani kwenye huduma hii ya usafiri wa mwendokasi.

“‘Mabasi hayo yamekuwa hayaeleweki mengi kutokuwa na  vipaza sauti vimekufa na kushindwa kuwatangazia abiria pia hayajulikani kama yanasimama vituo vya aina gani.

Yamekuwa yakisbabisha abiria wengi kupitilizwa vituo na kupata usumbufu mkubwa kwa kuwa abiria hawaelewi vizuri vituo vya mabasi.

Baadhi ya abiria wameomba vipaza sauti vitengenezwe kama ilivyokuwa awali ilikuwa ikitangazwa kabla yakufika kituoni abiria hutangaziwa kituo kinachofuata ili kuondoa usumbufu wa abiria kupilizwa vituo.

Abiria wa mabasi ya mwendokasi akiwa katika harakati za kuruka kutoka kwenye basi hilo kupitia mlongo ambao sio sahihi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *