Na Mwandishi Wetu

Mfanyakazi wa kampuni ya Aliburaq Ltd ambayo awali ilikuwa inafahamika kwa jina la SASCO Bw. Tumaini Amos (pichani), ameilalamikia kampuni hiyo kwa kumtelekeza baada ya kupata ajali mbaya ya gari akiwa kazini.

Akizungumza na Morningstar POST kwa masikitiko makubwa Bw. Amos alisema kuwa ameitaka kampuni hiyo kumwachisha kazi na kumlipa mafao yake ili kumsaidia kuendelea na matibabu.

Bw Amos alisema kuwa anashindwa kupata fedha za matibabu na kuitaka kampuni hiyo kumsaidia kwa kuwa amefanyakazi tangu mwaka 1980 akiwa na kampuni ya SASCO, ambayo mkurugenzi wake alikuwa anaitwa Seif Ali Salim.

Alisema kuwa mwanzoni mwa mwaka 2000 ilibadilika jina la kampuni hiyo kutoka SASCO na kuwa Aliburaq.

Bw Amos alisema kampuni hiyo imeshindwa kuendelea kumpa gharama za matibabu kwa kuwa hakuwa na bima wakati wa kupata ajali.

Aliongeza kuwa baada kupata ajali alipata matatizo ya mgongo hivyo zinahitajika.

Akizungumzia ajali hiyo Bw. Amos alisema kuwa mwaka 2021 mwezi Juni 6, alipata ajali mbaya ya gari akiwa na gari ya kampuni aina ya Benzi Actross 7769 DPW maeneo ya Monduli baada ya kugongana na roli na kuangukia porini.

Alisema baada ya kupata ajali kampuni yake ilimuhudumia akiwa Hosptali ya Rufaa ya Mkoa Tanga Bombo ambako alipata matibabu kadhaa, lakini baadae alhamishiwa hosptali ya Rufaa ya Muhimbili ambako walimtelekeza na mpaka sasa hana msaada wowote.

Bw Amos ameiomba kampuni hiyo kustaafu kwa kuwa amefika umri wa kustaafu kwa kuwa sasa ajali imempa ulemavu hawezi kufanya kazi tena, hivyo apatiwe mafao yake ili aweze kupatiwa matibabu ambayo yanahitaji gharama kubwa na kwa kuwa kampuni imeshindwa kumsaidia kulipia matibabu hayo.

Akijibu malalamiko hayon kwa njia ya simu kutoka Tanga, Mkurugenzi wa kampuni ya Aliburaq, Bw Yusuf Seif Ali hakutaka kuzungumzia zaidi suala la Amos kwa njia ya simu, hata hivyo Morningstar Post inaendelea kuutafuta zaidi uongozi wa kampuni hiyo kutoa ufafanuzi wa suala hilo la Amos zikiwemo taasisi za serikali zinahusika na haki za wafanyakazi.

0766600909

Mfanyakazi wa Aliburaq Bw Tumaini Amos anayeteseka nyumbani kwake baada ya kupata ajali akiwa kazi na  kutelekezwa na mwajiri wake, 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *