
Ushahdi wa kesi hii unasemaje?
Mara tu Chadema na mwenyekiti mshtakiwa na makamu wake walipoanza mkutano ya kuhamasisha no reforms no election msajili aliingilia kati ni ushahdi wa DW2 ni ushahidi wa John Mnyika na alisema kauli ya no reforms no election ilikuwa kauli ya kisiasa na akatoa taarifa kwa Umma na hiyo kabla ya tarehe tatu April na hiyo inaonesha msajili alikuwa tayari kuingilia na baadaye pia aliandika barua kwangu nikiwa tayari niko nguvuni na kesi ya uhaini.
Nimefunguliwa na hilo suala la msajili kuingilia halimo kabisa na jeshi la mawakili wa serikali na kwa mujibu wa sheria maana huwezi kufungua shauri la jinai kwenye jambo linaloweza kutatuliwa kimadai.
Kesi imefunguliwa bila kufuata sheria sababu walikuwa na haraka ya kuniua na kwa muktadha huo ni rai yangu kwamba mahakama hii itupilie mbali.
Hii kesi imefinguliwa kinyume cha sheria.
Hoja nyingine inayoonesha mashaka makubwa kuhusiana na kesi hii inahusu matumizi ya taratibu za kijanai kuendesha vita ya kisiasa kwa upande wa serikali.
Freeman Haikaeli Mbowe na viongozi wenzake saba wamelipishwa faini ya milioni 350 na mheshimiwa, mashahidi wote wa utetezi walikuja hapa walieleza miaka nenda rudi tunavyotengenezewa kesi wote walieleza walivyowekwa mahabusu wakashtakiwa.
Kesi yangu ya kwanza Christmas’s eve 22 wanangu ilikuwa krisimasi yao ya kwanza na wananiambia baba krisimasi yetu ya kwanza ulikuwa gerezani nimepewa kesi na Kikwete, Magufuli sasa nimepewa kubwa yenyewe na Samia.
Tumeteswa na makesi haya ya kisiasa tunagombania kuhusu mfumo wa uchaguzi sasa matumizi ya mifumo hii ya mashtaka na sheria inaturuhu kuikosoa na kupinga na hatulzimishwi na sheria kuwapenda.
Sheria inaturuhusu kuwa wapinzani na ninaposema sheria namaanisha katiba yetu na penal code inaturuhusu kuipinga kwa kila hali kupinga sera zake mifumo yake bila shida yoyote.
Hata kwenye mambo ya idara ya usalama wa taifa ambayo sheria imesema ni matishio kwa jamuhuri ya muungano, sheria hiyo imeweka wazi tukifanya harakati za kuiondoa serikali kwa kufuata taratibu hilo sio tishio la usalama wa taifa.
Sasa hii mchezo ya kutumia njia za kijinai dhidi ya washindani wa CCM huko sio kutenda haki hiyo ni political percecution.
Sasa waheshimiwa hizi kesi zinatakiwa zipigwe vita na mahakama inasemaje nianze na Freeman Haikael Mbowe mahakama hii ilikabiliwa na shtaka ambalo sio lake alikuwa amesema maneno ya yafuatayo ……Kesho patachimbika akakamatwa akashindwa kesi na mimi nilishtakiwa mara kibao maneno kama serikali imeiba hizo ni tuhuma sasa haziwezi tatuliwa kukamata watu na kuwafunga serikali ya kidemokrasia lazima ikubali na ivumilie ukosoaji wa kisiasa mimi nimepewa kesi ya uhaini kwa kusema maneno ambayo ni malalamiko ya kiuchaguzi wanataka hawa waendesha mashtaka na mapolisi wao wanataka iwe a police state kwa msimamo huohuo
Mahakama hii isikubali kuingilia mgogoro wa kisiasa uliogeuzwa kuwa jambo la kijinai.
Hoja yangu ya mwisho kwa mujibu shahidi DW2 aliyesema maneno haya amenifahamu kwa miaka 23 na kwamba ni mashtaka ya uongo mwingine ambaye amenifahamu kwa miaka 20 alisema mimi sio mtu ninayeweza kutenda uhaini na wote wanasema nimekuwa mhanga wa mabavu ya serikali ya Tanzania na sio rahisi kwa mzalendo kama mshtakiwa kuwa msaliti kwa nchi yake.
Hayo maneno sio ya machawa wangu hao sio machawa hao ni viongozi ambao nimefanya nao kazi nimepambana pamoja nao kupigania nao kupambania nchi yangu na kuthibitisha ushahidi ulioko mahakamani kwa rekodi yangu mbunge kwa kuchaguliwa rais wa TLS mshindi wa tuzo za kimataifa juu ya demokrasia na haki za binadamu.
Umoja wa Mataifa unasema niachiliwe na nilipwe fidia huyu ni mhaini wa aina gani anayepiganiwa na dunia nzima.
Nimepigania haki na demokrasia kwa shemu kubwa ya maisha yangu msimamo huo umenigharimu sana msimamo huo umeniletea madhila mengi sana msimamo huo kwa siku zilizobaki za maisha yangu nitaendelea kuupigania na kama ikibidi kufa ni msimamo ambao niko tayari kuufia.
Mwisho waheshimiwa majaji namalizia kosa la uhaini halina kosa dogo ambalo ukishindwa kuthibisha uhaini unaadhibu kosa dogo na adhabu yake kufa kunyongwa hadi kufa mzigo ambao uko mabegani mwenu ni kuamua kama kwa ushahidi huu mkiona kuna uhaini msigope kuadhibu sawa sawa na ilivyo.
Toeni hukumu inayostahili uhaini na kama hamjaona uhaini msiogope kusema hakuna uhaini hapa mshtakiwa hana hatia.
Kama kuna kosa hukumuni sawa sawa na ilivyo kwa mujibu wa sheria na kama ushahdi haufit basi futulieni mbali huo ni mzigo wa kwenu peke yenu. Mimi nimemaliza.
Tulipoanza niliijulisha mahakama kesi ya uhaini sio kesi rahisi na hata nyie mtakubali ukiachia mbali siasa zake na zinafanya uhaini kuwa kesi ngumu.
Pamoja na magumu yote ya kesi hii, mmetusikiliza mmetupa nafasi ya kujieleza mmenipa nafasi ya kujitetea mmetuvumilia mmefanya kazi nzuri na nilitaka niseme haya sababu sijui kama tutakutana tena kwenye mazingira haya na hawa mawakili wangu wa serikali wamepambana vyovyote mtakavyo amua nawapa pongezi nawatakieni kila la kheri kwenye tafakari yenu.
Ahsanteni sana hayo ndio nilitaka yaingie kwenye rekodi waheshimiwa majaji.