NA MWANDISHI WETU
Beki wa zamani wa Simba SC na Singida Big Stars, Israel Mwenda, ametua rasmi Yanga SC, mabingwa
mara 30 wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Mwenda, mwenye uwezo wa kucheza kama beki wa kulia (namba 2) na kushoto (namba 3), amemaliza
msimu mfupi na Singida Big Stars kabla ya kujiunga na Wanajangwani.
Usajili wake unatarajiwa kuongeza ushindani kwenye safu ya ulinzi, hasa dhidi ya Kouassi Yao, ambaye
amekuwa chaguo la kwanza katika nafasi ya beki.