NA MWANDISHI WETU
Ripoti ya Makadirio ya Ukuaji wa Uchumi ya Benki ya Dunia (WB) imeonesha Uchumi wa Kenya utashuka katika Ukuaji wake kutoka 5.0% ya makadirio ya awali hadi 4.7%.
Mafuriko, Maandamano dhidi ya Serikali na Juhudi hasi za Uimarishaji wa Uchumi vikitajwa kuathiri ukuaji huo.
Pia, ripoti imeonesha Kenya bado inakabiliwa na hatari kubwa ya kuelemewa na mzigo wa Madeni huku Deni la Serikali likizidi kuwa dhaifu ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa gharama za kulipa deni hilo pamoja na kukosa malengo ya mapato.
Aidha, WB imeitaka Serikali kukabiliana na hali ya kukosekana kwa usawa wa Kimuundo ambayo imetajwa kuwa chanzo cha kufifisha malengo ya ukuaji endelevu na shirikishi wa Uchumi.