Kiongozi wa Chama cha  Demokrasia na Maendeleo   Chadema, akihutubia wakazi wa Mbezi Luis ambao hakuwa na watu wengi wanaosikiliza mkutanoni hapo, siku ya jumapili tar 24 mwaka huu (Picha Na Barnaba Chilunda Mbezi Luis).

Na Jones Mwang’onda

Wakazi wa Mbezi Luis jijini Dar es Salaam, katika hali ya kushangaza walisusia kuhudhuria mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, uliofanyika maeneo ya Mbezi Luis kwenye makutano ya barabara ya Goba na Morogoro majira ya alasiri jumapili iliyopita.

Mkutano huo uliofanyika katika maeneo hayo na kuhudhuliwa na Katibu Mkuu wa Chadema, Bw. John Mnyika ulikosa kabisa watu wa kusikiliza na wengi hawakuweza kufika katika mkutano huo.

Mkutano huo ulianza majira ya saa tisa alasiri kwa viongozi wa chama hicho kuanza kuzungumza na watu ambao walionekana mmoja mmoja wengi walikuwa ni wapita njia ambao hawakuwa wakisikiliza.

Wakizungumza katika mkutano huo viongozi wa Chadema ambao walionekana kuzungumza zaidi maneno ya kashfa dhidi ya Chama cha Mapinduzi CCM, hatua hiyo iliwakera baadhi ya watu wachache waliokuwa kwenye mkutano huo ambao walianza kuondoka eneo la mkutano.

Mkutano huo ambao ulikuwa wa amani na utulivu kukiwa na hali ya usalama lakini viongozi wa chadema waliokuwa wakizungumzia masuala ya Uwekezaji wa bandari,  Katiba mpya pamoja na ufisadi na kuwataka wananchi wa mbezi kutokuiamini serikali ya CCM.

Viongozi wa Chadema walikuwa wakizungumza maneno machafu ambayo hayastahili kuchapishwa ambayo yaliwakera wananchi wachache waliokuwepo ambao walianza kuondoka eneo hilo.

Katika mkutano huo polisi waliokuwa wanalinda amani katika mkutano huo walionesha weledi wakiwa kwenye gari lao walifanya kazi kwa maadili makubwa kwani hata gari lao liliegeshwa mbali karibu na ofisi za polisi jamii za eneo hilo.

Baadhi ya wananchi waliwataka polisi kwenda kuwakamata viongozi wa Chadema waliokuwa wakitumia maneno  machafu na  matusi, lakini polisi walitumia weledi na busara kuhakikisha amani inatawala.

Mzee mmoja wa Mbezi Luis aliyekuwa katika mkutano huo aliyejitambulisha kwa jina Mzee Hadhuruni, alisema wanataka siasa za amani zitakazosaidia kuleta maendeleo ya nchi.

Mzee Mchungu akizungumzia jambo hilo alisema wanasiasa wanamuonea Rais Samia Suluhu Hassan alihoji kwa nini mambo hayo yanayofanyika sasa wasingeyafanya wakati wa hayati  Magufuli.

Mwingine mzee maarufu Mbezi Luis mzee Zengwe, alisema angekuwa na uwezo angeiomba serikali kupiga marufuku mikutano ya hadhara kwani inaweza kuchochea vurugu katika nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *