Harakati za uokoaji baada ya kulipuka kwa moto zinazofanywa na kikosi cha uokoaji

Na Jones Mwan’gonda na Fred Okoth

Uchunguzi wa Gazeti hili la mtandao umebaini kwamba
Baadhi ya Watendaji wa ardhi kwenye Manispaa jijini Dar es Salaam ni chanzo kikubwa cha majanga yanayotokea kwenye sekta hiyo, Morningstar POST imebaini.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili la Mtandaoni la Morningstar Post umebaini kuwa kila mara yanapotokea majanga ya moto kama yaliotokea juzi hapa jijini Dar es es Salaam yanatokana kuwepo migogoro mingi ya
ardhi na ujenzi holela uliokithiri hapa nchini.

Morningstar Post imebaini
kuwa baadhi ya watendaji wa ardhi hawafuati sheria za ardhi na wanakula rushwa
kuruhusu watu kujenga majengo kiholela.

Miaka ya nyuma kidogo, Jiji la Dar es Salaam lilishuhudia
maporomoko ya maghorofa matano  ambapo mwaka 2013,
ghorofa lililokuwa mtaa wa Indira Ghandi liliporomoka na karibu watu 34 kupoteza maisha ilitokana na kufanywa kwa ujenzi holela na baadhi ya viongozi husika wakati huo walikuwepo  na hawafanyi lolote.

Uchunguzi wetu imebaini kutokowepo usimamizi wa kutosha katika sekta ya ujenzi nchini pamoja na watu kufanya biashara ya vifaa vya ujenzi kiholela nchini.

Biashara hizo ni pamoja na kuwepo utengenezaji wa matofali yasioyokuwa na viwango
kutokana na kutokwepo usimamizi mbovu katika sekta ya ujenzi.

Afisa mmoja wa benki ya CRB ambaye hakupenda kutaja jina lake akiongea na waandishi wa habari hizi, alisema ni muhimu sekta husika ikafanya haraka
ukaguzi mkali katika vifaa vyote kuanzia matofali kwa
sababu vingi havina viwango hata kidogo.

“ Matofali mengine ni kaburi kwa kweli,” alisema.

Kipindi cha mvua, Dar es Salaam hukumbwa na adhaa ya
makazi na mitaa hufurika maji tatizo kubwa likiwa ni miundo mbinu na watu kujenga makazi kwenye njia za maji.

“Embu pita tu pale Kariakoo uone jinsi nyumba
zinavyobadilishwa, vichochoro vyote sasa ni viduka, ghorofa
zinabadilishwa kutoka makazi kuwa maduka kimya kimya,
ujenzi unafanyika nyakati za usiku tu, wasimamizi wa sheria
hawapo au wamebariki?” alihoji mkazi mmoja Kinondoni ambaye
hakutaka jina lake lichapishwe.

“Haiwezekani twende tu kama wanyama, matokeo yake si
mazuri. Hapakuwa na haja ya kuondoa machinga kisha
kuruhusu hizo sehemu za wamachinga kujengwa ngazi za
kupandia juu au kujenga vibanda vya mabati na kugusanisha
na ukuta wa nyumba halafu mnasema ni halali?” aliendelea
kuhoji.

“Huu ni uozo unaosubiri kunuka wakati wowote. Kuta za
maghorofa zimegusana kiasi hata paka hawezi kupita, ujenzi huu
unapatikana Dar es Salaam peke yake.” alisema kwa masikitiko.

Hali halisi ya mazingira ya jiji hili kwa sasa ni mbaya, na baadhi
ya wakazi wameingiwa na hofu ya kutokea maafa makubwa
katika msimu huu unatabiriwa kuwa na mvua za el-ninyo.

Mvua zilizonyesha hivi karibuni jijini humu, zimejengea hofu
kwa wakazi wa jiji hili kutokana na madhara yalitokea ikiwemo
baadhi ya nyumba na kuta kubomoka, maeneo kusambaa ya
makazi kujaa maji, na maji kulazimisha kupita kwenye nyumba baada ya njia zake za asili kuzibwa.

Pamoja na wakazi waliojenga kwenye njia za asili za mapito ya
maji, yakiwemo mabonde na makorongo, uongozi wa jiji hili pia unapitia maeneo yote yaliyokuwa yametengwa kama maeneo ya wazi, ili uweze kuchukua hatua pale sheria itakapokuwa imekiukwa.

Kutokana na ujenzi holela, kila mtu hujichukulia sheria mkononi, kwa kujenga anavyoona inampendeza, hivyo kila mmoja
hujitahidi kuzuia maji yasiingie kwako, na kwa utaratibu huo
maji yamekosa sehemu za kupita.

Takribani kila mkazi wa Jiji hili utakayemuliza kuhusu
kinachomkera zaidi, atakujibu kuwa ni ujenzi holela na wote
huwanyoshea vidole viongozi wa jiji hili waliokuwepo.
Wanasema ujenzi holela umesababisha maji kushindwa kupita
kwenye mikondo yake ya asili, na hulazimika kutafuta njia
zingine.

“Ujenzi holela ni matunda ya idara ya mipango miji,
hawasimamii vema, sijui wamesomea kuharibu au kupanga
miji,” alisema mama Lucy wa Sinza.

Moja ya sababu inayotolewa na wataalamu wa jiji hili kuhusu
kushamiri kwa ujenzi holela ni ufinyu wa bajeti kwa ajili ya
kupima viwanja.

Hata hivyo, kauli hiyo inapingana na wakazi wengi wa jiji hulaumu wataalamu wa mipango miji kwa kuendekeza
rushwa. Wakazi hao wanadai kuwepo sehemu jijini humu
ambazo wananchi wako tayari kujitolea lakini hawapati
ushirikiano kutoka jiji.

“Wanagawana viwanja kumi kumi na kuwauzia watu, mipango
miji shida kweli kweli, hata Mama Samia ana kazi kubwa ya
kufanya na hawamuungi mkono maafisa wengi,
wanamshangaa, kwao miji holela ndio biashara na raha yao,” alisema mkazi mwingne wa Mbagala  aliomba  jina lake lisitajwe .

Wakazi wengi wanalalamikia rushwa kukithiri kwenye suala la
viwanja kwa ajili ya makazi, na kwamba ndio iliyochangia kwa
wenye pesa kuvamia maeneo ya wazi na barabara za mitaa.

Hatua ya kuondoa makazi kwenye mapito ya asili ya maji na
maeneo ya wazi ni nzuri kwa ustawi wa jiji hili pamoja na
kuepusha maafa kwa wakazi wake, lakini mtihani unabakia kwa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya jiji hili, iwapo watakuwa tayari kupoteza umaarufu walionao mbele ya wapiga kura wao kwa kusimamia sheria za ardhi.

Hivi karibuni moto ulilibuka maeneo ya soko la Karikoo katibu na kituo cha mafuta cha Big Born.

Hatua hiyo ya moto imekuja baada ya Morningstar kuripoti hivi karibuni kuhusu ujenzi wa jengo la chini lililojengwa maeneo hayo na mkurungenzi wa jiji kukanusha kuvunja sheria ya mipango miji.

Taarifa ya awali

Halmashauri ya jiji la Dar es salaam, imeshindwa kusimamia sheria ya mipango miji inayoelekeza uendelezaji wa majengo ya juu katika maeneo ya katikati ya jiji la Dar es salaam.

Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na blog hii umebaini kuwa majengo mengi ya chini yasiyotakiwa kujengwa yanashamiri kujengwa katikati ya jiji hususani katika maeneo ya Kariakoo.

Katika barabara ya Msimbazi maeneo ya kituo cha mafuta cha Big Bon, kumejengwa jengo la chini ambalo hapo awali halikuwepo kinyume na sheria ya mipango miji inayoelekeza halmashauri kusimamia ujenzi wa majengo ya juu katikati ya jiji kukabiliana na ongezeko la ujenzi holela.

Akizungumza na Morningstar Post, Mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam, Bw Amani Mafuru, alishindwa kutoa maelezo kuhusu jengo hilo, lililojengwa maeneo ya Msimbazi kwenye kituo cha mafuta cha Big Bon.

“Mimi ni Mkurugenzi sihusiki na mambo yanayofanyika kwenye field, hapa kwangu kuna kuja mafaili zaidi ya mia sita kila siku ntafahamu vipi mambo yanayofanyika huko nje,” alisema.

Bw. Amani alisema hapaswi kulaumiwa wala kutuhumiwa  kwa makosa yanayofanywa na watendaji wake wa chini kama kuna makosa yoyote yanafanyika mkurugenzi hapaswi kutuhumiwa yeye bali inapaswa kuhushwa ni ofisi yake.

Akaongeza kuwa kuhusu ufafanuzi wa jengo hilo lililojengwa kwenye kituo cha mafuta cha BigBon atafuatilia kwa watendaji wake wa  chini yake na kutoa ufafanuzi kuhusu jengo hilo baadae.

Akasisitiza zaidi kuwa yeye hapaswi kutuhumiwa kwa makosa yanayofanywa na watendaji wake wa chini, malalamiko na tuhuma zote zinapaswa kuelekezwa kwenye ofisi ya mkurugenzi na sio mkurugenzi.

Mkurugezi alitoa ufafanuzi huo kufuatia maswali yalioelekezwa kwake na Morningstar Post yakimtuhumu mkurugenzi na injini wa jiji kuhusika kwa uvunjifu wa sheria ya mipango miji kwa kuruhusu majengo ya chini kuendelea kujengwa katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Uchunguzi wa Morningstar Post umebaini kuwa majengo mengi ya chini yanayojengwa katikati ya jiji la Dar es salaam hayana vibali au yanakuwa yanatumia vibali vya ukarabati vinavyotolewa na halmashauri na kuanzisha ujenzi mpya.Hali ambayo inashindwa kusimamiwa na watendaji wa halmashauri kuanzia ngazi ya kata.

Kwa mujibu wa sheri ya mipango miji inaelekeza wazi kutotolewa kwa vibali vipya vya ujenzi wa majengo ya chini katika maeno ya katikati ya jiji la Dar esa Salaam badala yake jiji liendelezwe kwa ujenzi wa majengo ya juu.

Kutokana na uhitaji mkubwa wa maduka ya biashara wamiliki wengi wa nyumba hususani katika maeneo ya karikaoo wanashindwa kujenga majengo ya juu badala yake wanatumia vibali vya ukarabati kujenga fremu za maduka.

Soko la Kariakoo lililowaka moto hivi karibuni

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *