WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali itaendelea kutekeleza miradi ya maendeleo iliyoahidiwa katika Mkoa wa Singida, ikiwemo barabara, reli ya kisasa (SGR), uwanja wa ndege pamoja na miradi ya maji, afya na elimu kwa lengo la kuchochea maendeleo ya wananchi na kukuza uchumi wa Taifa.

Ametoa kauli hiyo alipohutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Maonesho wa Mandewa, wilayani Ikungi, mkoani Singida, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo.

Waziri Mkuu amesema Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amemtuma kuwahakikishia wananchi wa Mkoa wa Singida kuwa miradi yote ya maendeleo iliyoahidiwa itaendelea kutekelezwa hatua kwa hatua kwa kuzingatia vipaumbele vya Serikali.

“Mheshimiwa Rais amenituma niwahakikishie kwamba mambo ambayo wabunge wenu wamekuwa wakiyasema na ambayo aliwaahidi wananchi wa Singida yatakwenda kutekelezwa,” amesema.

Amesema Serikali itaendelea kutekeleza miradi ya barabara ikiwemo Sabasaba–Sepuka–Ndago–Kizaga, Njia Panda–Makiungu–Mungaa–Misughaa–Ndago, Mkiwa–Itigi–Rungwa–Makongorosi, Iguguno–Nduguti–Sibiti, pamoja na Singida–Ilongero–Haydom, hatua zitakazorahisisha usafirishaji, biashara na kufungua fursa zaidi za kiuchumi katika Mkoa wa Singida na maeneo jirani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *