NA MWANDISHI WETU

Baada ya kuwa umetengeneza jukwaa lako la group la whatsapp, umerusha tangazo watu wamekuja kwenye jukwaa, sasa ni wakati wa kuuza bidhaa au huduma yako.

*Nini unatakwa kufanya ili kuuza kwa wingi?*

Kumbuka kuwa watu wanapoona tangazo lako mtandaoni, na kubofya linki kuingia kwenye jukwaa lako, wanakuwa wameonesha shauku ya kununua bidhaa au huduma yako.

Kinachoweza kufanya washindwe kuchukua hatua ya kununua bidhaa au huduma yako, ni hofu ya kutokupata matokeo, kutapeliwa, kufanya makosa kupoteza pesa, muda au kukosolewa.

Ili kuvunja hofu ya walengwa kuchukua hatua, unatakiwa kutoa kitu cha bure kwa walengwa wako kabla ya kutaka kuwauzia bidhaa au huduma yako, kitu cha bure kinaweza kuwa ushauri, mafunzo au dondoa za kuwasaidia kuboresha maisha yao.

Ukiweza kufanya vizuri katika hatua hii kufanya mauzo kwenye jukwaa lako inakuwa ni kazi rahisi.

*Jinsi ya kutoa kitu cha bure ndani ya jukwaa*

Unaweza kutoa ushauri, mafunzo au dondoo za bure kwa walengwa wako kwa njia ya makala, sauti au video ili kujenga uaminifu, kutengeneza mahusiano, kuwafanya walengwa wako wakujue, wakupende na kukuamini ili kununua bidhaa au huduma yako.

Unapotoa ushauri kwa walengwa wako katika namna ya kuibua shauku kuchukua hatua, kununua bidhaa au huduma yako, unatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo:

*1. Kujua vizuri haswa changamoto ya walengwa wako ni ipi?*
*2. Kujua ukubwa wa tatizo na madhara yanaweza kuwapata walengwa*
*3. Kujua vizuri haswa bidhaa au huduma yako inavyoweza kuwasaidia walengwa wako.*

Kama hujafahamu vizuri walengwa wako ni kina nani, wana changamoto gani, bidhaa au huduma yako inaweza kuwasaidia vipi walengwa wako, kutengeneza makala, ushauri au dondoo za kugusa hisia za walengwa wako itakuwa kwako ni changamoto.

*Jinsi ya kutengeneza ujumbe, ushauri au makala za kuibua shauku*

Hatua ya kwanza anza kwa kueleza matatizo yanayowakabili walengwa wako, kwa mfano kama unauza nguo, unaweza kuanza kwa kueleza kama ifauatavyo:

Kama wewe ni kijana unayeahangaika kutafuta nguo zinazokwenda na ‘fashion’, unahitaji nguo zinazokwenda na wakati.

Hapo unakuwa umeeleza tatizo la kile ambacho mlengwa wako anakitamani, anakihitaji ambacho anataka suluhisho.

Baada ya kueleza tatizo unatakiwa kueleza ukubwa wa tatizo, iwapo mlengwa wako atashindwa kuchukua hatua ni madhara gani yanaweza kumpata.

Mfano, kama unashindwa kupata sehemu sahihi ya kupata nguo za ‘fashion’ na zinazokwenda na wakati, maana yake utaendelea kupoteza pesa na muda wako mwingi.

Hatua ya tatu ni kueleza faida ya kile ambacho bidhaa au huduma yako inafanya, iwapo mlengwa wako atachukua hatua ya kununua kwako.

Mfano, unaweza kueleza kama unasoma makala haya au unasikiliza ‘clip’ hii au unaangalia video hii, habari njema leo ntakueleza aina za nguo za ‘fashion’ kwa wanawake zinazokwenda na wakati.

Unaweza kueleza kisha ukamwambia kuwa achukue hatua kama atapenda kupata nguo hizo, anaweza kutuma ujumbe WhatsApp au kupiga simu, ukaeleza hatua ambayo unataka achukua baada ya kujua faida ya bidhaa au huduma yako.

Kwa kufanya hivyo ndani ya jukwaa lako unaibua shauku ya walengwa kununua, unajenga uaminifu kwao, hivyo kufanya mauzo inakuwa ni jambo rahisi.

Kwa hivyo ni muhimu sana kujua mlengwa wako ni nani, kujifunza kwa kina bidhaa au huduma unayotoa inawezaje kumsaidia mteja wako, na faida anazoweza kupata baada ya kutumia.

Usiingie majaribu ya kutaka kuuza bidhaa au huduma yako mara tu walengwa wako wanapoingia kwenye jukwaa bila kujenga uaminifu kwanza.

0765868582

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *