BBC

Ingawa alitarajiwa kustaafu soka ya kimataifa baada ya Kombe la Dunia lililopita, gwiji wa Ureno, Christianto Ronaldo bado ana ushawishi mkubwa na atacheza kuwania ubingwa wa Ulaya kwa mara ya sita msimu huu nchini Ujerumani.

“Nilikutana na Ronaldo nilipokuwa nikifundisha Everton mwaka 2013,” meneja wa Ureno, Roberto Martinez anasema.

“Inavutia kwa umri wake ila bado ana tabia na hamu ya kijana wa miaka 18. Ana mawazo na hana mipaka. Amekuwa na timu ya taifa kwa miaka 20 sasa.”

Licha ya kuwa na umri wa miaka 39, Ronaldo ameonyesha hana mpango wa kuondoka katika soka la kimataifa.

Nyota huyo wa zamani wa Manchester United amemwambia Martinez lengo lake ni kufikisha mechi 250 akichezea Ureno. Kwa sasa ana mechi 207.

Ili kufanikisha hilo, atalazimika kukabiliana na ukosoaji unaoongezeka kutoka kwa mashabiki wa nyumbani ambao wanaamini Ureno inafanya vizuri zaidi bila yeye.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *