Na Mwandishi Wetu, Lindi

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh.Samia Suluhu Hassan amewashauri wananchi wa Somanga Kusini wilayani Kilwa mkoani Lindi kuwa na subira ya kupata nishati ya umeme.

Mh. Rais Samia aliwataka wananchi hao kuwa na subira ya miezi 18 hadi 20, ili kuondokana na changamoto ya nishati ya umeme na huduma ya maji.

Rais Samia ameyasema hayo alipozungumza na wananchi hao na kusema pia changamoto za wafugaji na masuala ya ardhi serikali itafanyia  kazi.

Rais Samia alisema kwamba serikali itashughulikia suala la maji kwa vijiji 50 kupata huduma ya maji wilayani humo

Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kaskazini, Francis Ndulane aliishukuru serikali kwa kutekeleza miradi ya maendeleo kwenye sekta za afya, barabara na maji.

Rais Samia Suluhu Hassan

Rais Samia Suluhu Hassan

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *