
.
Katuga: Waambue majaji, uliposema kukinukisha ni kupika pilau?
Brenda: Hakuelekeza kupika pilau.
Katuga: Sasa mapilau yalitoka wapi?
Brenda: Ukizuia uchaguzi, watu watajua.
Katuga: Je, katika ushahidi wako ulisema jinsi gani mwenyekiti alitaka mkinukishe?
Brenda: Sikusema.
Katuga: Katika ushahidi wako uliwaambia majaji kuwa mliambiwa mfanye moja, mbili, tatu…
Brenda: Sikusema.
Katuga: Katika ushahidi wako ulisema njia Lissu alizowaelekeza kuzuia uchaguzi?
Brenda: Sijasema.
Katuga: Kwa kuwa umesomewa mara kadhaa haya maneno kuwa Lissu alitumia ili kuweza kuzuia uchaguzi, ni ushahidi muhimu kuusema au si ushahidi muhimu?
Brenda: Ni ushahidi muhimu.
Katuga: Waambie majaji kama kuchoma vituo vya kupigia kura na karatasi za kupigia kura inaweza kuwa ni kitendo cha kuzuia uchaguzi.
Brenda: Ni sahihi.
Katuga: Waambie majaji kama kuchoma mali ya umma kunaweza kuvunja amani na kuzuia uchaguzi.
Brenda: Ni sahihi.
Katuga: Waambie majaji kama kukata wapiga kura vidole kunaweza kuzuia uchaguzi.
Brenda: Sahihi.
Katuga: Waambie majaji kama ulimsikia mwenyekiti akisema, “Ama tutazuia huu uchaguzi kwa kufungua kesi mahakamani.”
Brenda: Sikumsikia.
Katuga: Ulisema CHADEMA inaamini katika demokrasia?
Brenda: Ndiyo.
Katuga: Kwa kuwa mnaamini demokrasia, ni haki vyama vingine kushiriki uchaguzi?
Brenda: Ndiyo.
Katuga: Ni haki ya kikatiba?
Brenda: Ndiyo.
Katuga: Na si haki kumzuia mtu kushiriki uchaguzi?
Brenda: Si haki.
Katuga: Na vilevile si haki mtu kuhamasisha watu wengi kumzuia mtu anayetaka kushiriki uchaguzi, na ni kosa kisheria?
Brenda: Si haki.