Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) amezindua Kampeni za Chama Cha Mapinduzi CCM ndani ya Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Kisiwani Unguja.

Mkoa huo unajumuisha kwa Majimbo Manne, ambapo Jimbo la kikwajuni, Kwa nafasi ya Mgombea Ubunge ni Eng. Hamad Yussuf Masauni na Muwakilishi ni Seif Kombo Pandu, Jimbo la Kwahani Mgombea Ubunge ni Mohammed Abdalla Laki na Muwakilishi Mohammed Sijiamini Mohammed, Jimbo la Jangombe Mgombea Ubunge ni Ali Abdullgullam na Uwakilishi ni Ali Hassan King, Jimbo la Malindi Mgombea Ubunge ni Muhsini Haji Ussi na Muwakilishi ni Abdulghani Issmail Zubeir. Mwaki.

Katika uzinduzi huo ulijumuisha pia Madiwani wa Kata Kumi na Mbili (12) Chatanda alitumia Jukwaa Hilo kwa kuwanadi Wagombea hao na kuwaombea kura za kishindo kuelekea Uchaguzi Mkuu hapo Oktoba 29, 2025, pamoja na Kumnadi Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa upande wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa upande wa Zanzibar.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *