*JE BIASHARA NI NINI ?*
_Biashara gani yenye kulipa mtandaoni?_
_Je unawezaje kuanza biashara bila mtaji?_

Na Mwandishi Wetu

Watu wengi ukiwauliza biashara ni nini watakuletea maelezo yanayofundishwa kwenye vyuo na sehemu mbalimbali kuwa biashara ni kuuza na kununua huduma au bidhaa.

Ni kweli hii ndiyo tafsiri na maana halisi ya biashara lazima kuwepo na muamala wa kuuza na kununua bidhaa au huduma kwa mabadilishano ya fedha au bidhaa.

Hata hivyo, ukienda mbali zaidi na kuchunguza kwa kina maana ya biashara kama ambavyo wajasilimali wakubwa dunia kama vile Brayn Trace anasema biashara ni ile yenye kuleta utatuzi wa matatizo ya walengwa wako.

Kimsingi, biashara ambayo haiwezi kutatua matatizo au changamoto za watu au walengwa hii ni biashara iliyokufa haiwezi kupiga hatua na kukua katika kiwango kizuri na kuleta mafanikio.

Wateja au watu wanaonunua bidhaa au huduma hawanunui kwa sababu wanahitaji kununua kutoka kwako bali wananunua ili kutatua matatizo yao.

Biashara ziko za aina nyingi lakini katika makala haya ntaeleza aina moja ya biashara ambayo ni biashara isiyohitaji mtaji mkubwa na jinsi unavyoweza kufanya biashara bila mtaji au kwa mtaji mdogo sana.

Ninapozungumzia bila mtaji naomba nieleweke kuwa mtaji umegawanyika katika namna tofauti, kuna mtaji wa uendeshaji, (running capital), mtaji wa uwekezaji (investment capital) kuna mtaji wa rasilimali (asset capital) nk.

Hapa nazungumzia kuanzisha biashara bila mtaji wa uendeshaji lakini utahitaji mtaji wa nguvu kazi ambayo kwa asilimia 100 wewe mwenye unaweza kuwa mtaji.

Kila kitu unachotakiwa kufanya katika biashara ni mtaji, unapotenga muda wa kushughulikia na biashara yako ni mtaji, unapotumia nguvu zako kutengeneza biashara yako ni mtaji. Mtaji mkubwa ni wewe.

*Je biashara gani yenye kulipa ?*

Biashara ya kitaalam, wengi wakisikia neno mtaalam wanaopata hisia za kuwa na vyeti vya diploma au degree. Ni kweli kuwa mtu aliyehitimu mafunzo na kutunukiwa vyeti anaweza kuwa mtaalam.

Lakini pia mtu anyefahamu jambo fulani kwa kina bila ya kuwa na cheti pia anaweza kuwa mtaalam. Mfano wavuvi wangapi wanavua samaki lakini hawana vyeti vya uvuvi hao ni wataalam wa kuvua samaki.

Si maanishi hakuna umuhimu wa kusoma na kuwa na vyeti vya taaluma fulani nachozungumzia ni maana ya utaalam. Kabla sijazama ‘deep’ kueleza biashara ya kitaalam nieleze kwa kifupi utaalam ni nini.

Mtaalam ni mtu mwenye ujuzi wa juu au maarifa fulani ya jambo fulani mfano masoko, tiba, aina hiyo ya ujuzi au maarifa inatokana na kujifunza katika njia rasmi shuleni au vyuoni au njia isiyo rasmi ya kusoma vitabu kufanya kwa vitendo au uzoefu wa kazi.

*Biashara ya kitaalam ni ipi?*

Kuwa na biashara ya kitaalam ni namna ya kubadilisha elimu, ujuzi au maarifa uliyonayo kuwa fursa ya kujipatia kipato kwa kuanzisha huduma au bidhaa kuhusiana na utaalam wako.

Aina hii ya biashara ni ya kipekee na mbinu ya kutoa maarifa uliyonayo kwa kundi fulani la watu kupitia kutoa elimu ya kile ulicho na utaalam nacho unakuwa wa kipekee na hakuna mshindani.

Biashara ya kitaalam inaweza kujengwa katika ujuzi na maarifa mbalimbali kama jinsi ya kutengeneza tovuti, jinsi ya kupika, jinsi ya kutoa tiba fulani, jinsi ya kutengeza bidhaa nk.

Vile vile biashara ya kitaalam inaweza kuelezwa kwa namna tofauti mfumo tofauti mfano.Ushauri (consultation) Ualimu, kochi (Coaching) Uzungumzaji (Speaking) Mafunzo (Training).

Jinsi ya kuanzisha biashara bila mtaji unahitaji kufahamu aina hii ya biashara ya kitaalam kwani haihitaji mtaji mkubwa kama ambavyo unavyoweza kuuza bidhaa za kawaida.

Unachotakiwa kufanya kuweza kuanzisha biashara ya kitaalam ni kufanya utafiti wa soko na kubaini changamoto zinazowakabiili walengwa wako, baada ya hapo ni kujifunza na upata suluhisho la matatizo yao na kuanza kuwauzia utatuzi wa matatizo yao.

Nirahis sana kuanza kufanya biashara ya kitaalam bila kuwa mtaji mkubwa, awali unaweza kuanza kujaribu wazo lako kwa watu wachache likifanya kazi unaingia kwenye biashara.

nicheki whatsapp
0765868582

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *