
Kiungo wa zamani wa Simba, raia wa Brazil Gerson Fraga Vieira,
Na Mdoe Kiligo
JAMAA amegoma kuondoka kabisa Simba! Ndivyo unavyoweza kuandika kama unataka kuzungumzia ukweli.
Nyota wa zamani wa klabu ya Simba SC ya Tanzania mbrazil Gerson Fraga Vieira aliondoka Simba muda mrefu sasa, lakini pamoja na kuchezea timu tofauti baada ya kuondoka mtaa wa Maimbazi hajabadili picha kwenye ‘profile’ yake mpaka sasa ambayo aliiweka akiwa na Wekundu hao wa Msimbazi.
Washabiki wenyewe wa Simba wanasema katika maoni yao kwa Fraga kwwmba hayo ni mahaba makubwa ambayo kiungo huyo anayo katika klabu yao hiyo. Fraga hivi karibuni ameongeza mkataba wa kuendelea kusalia kwenye klabu ya Tai Po FC ya huko Hong Kong kisiwa kinachomilikiwa na China
Lakini sasa atakuwa na majukumu mawili tofauti atakuwa kama kocha mchezaji kwenye klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ambayo msimu uliopita walimaliza kwenye nafasi ya pili.