Wanafunzi wa shule ya Sunrise wakiwa kwenye tamasha la michezo la kila mwaka aliyeko katikati ni Maua mtoto wa aliyekuwa waziri wa serikali ya awamu ya nne Maua Daftari

Wazazi wakiwa na wanafunzi kwenye tamasha la michezo la kila mwaka la shule za Sunrise lilifanyika leo viwanja vya Leaders Club

Na Omar Mbarak

Tamasha la michezo la kila mwaka la  shule za Sunrize lililofanyika leo kwenye viwanja Leaders Club Kinondoni, jijini Dar es Salaam, limewavutia watu wengi waliohudhulia tamasha hilo.

Katika tamasha hilo lililoanza asubuhi ya leo kwa kufanyika michezo ya aina mbalimbali.

Katika mchezo wa mpira miguu , mchezaji wa mpira wa miguu shule za Sunrise, Simon Bishanga amekuwa kivutio kikubwa katika tamasha la michezo ya kila mwaka lililofanyika katika viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Simoni kijana mdogo kutoka katika kundi la Gold alionekana kuwa nyota wa michezo hiyo baada ya kunesha mchezo mzuri na kubahatika kufunga goli katika mchezo.

Katika tamasha hilo wanafunzi waligawanywa katika makundi mbalimbali walioshiriki michezo kwenye tamasha hilo ikiwa ni pamoja na kundi la Gold, Silver, Platinum nk

Tamasha hilo lilihudhuliwa na watu mbalimbali wakiwemo wazazi lililenga kujenga afya za watoto na kudumisha mahusiano mazuri kati ya wanafunzi na wazazi na viongozi wao.

Katika mchezo wa riadha ambayo ilifanya kwa makundi tofauti, moja wa mbio hizo mtoto wa aliyekuwa waziri mstaafu Maua Daftari alishinda mbio hizo.

Katika tamasha hilo ilifanyika michezo mbalimbali kama vile kuruka kamba, kucheza, kupuliza maputo, mbio za magunia, kuvuta kamba na mingine mingi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *