KOCHA wa Simba, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema kipigo cha mabao 5-1 walichopata kutoka kwa watani Yanga ni sehemu ya mpira.
Robertinho amesema kipindi cha pili walipoteza umakini na kushindwa kuzuia nafasi ambazo wapinzani wao Yanga walizitumia vizuri.
Aidha, Robertinho amesema hawakuwa vizuri wakati wanapopoteza mpira na wapinzani waliweza kuwasoma na kutumia madhaifu yao kuwa faida kwa Wananchi.
“Nawapongeza wapinzani kwa ushindi hatukuwa vizuri hasa kipindi cha pili lakini huu ni mpira na tunajipanga kwa mchezo ujao,” amesema Robertinho.