Win Kapama

Na MWANDISHI WETU

Kufuatia Polisi wa Kituo cha Oysterbay jijini Dar es Salaam, kugoma kutekeleza amri ya Mahakama Kuu, ndugu wa mtuhumiwa wamemuomba Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuingilia kati suala hilo.

Hivi karibuni Mahakama Kuu mbele ya jaji W.P Ndyansobera Oktoba 19, mwaka huu, iliamuri polisi kumwachia Zakaria Antony Kapama aliyekamatwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay na kuwekwa mahabusu kinyume na sheria lakini mpaka tunapoandika habari hizi bado ajaachiwa huru.

Akizungumza na Morningstar Post, kwa niaba ya familia, Bi Winnie Kapama (pichani), alisema wanamuomba Rais Samia kuingilia kati suala hilo kwa kuwa sheria za nchi zinakiukwa na jeshi la polisi.

Bi. Win alisema kuwa polisi hawatendi haki kwa kuwa wanaendelea kumshikilia licha ya kuwa amri ya Mahakama Kuu imeamuru kuachiwa huru.

Alisema kuwa familia yao inawasiwasi kuwa huenda kuna polisi mmoja mkubwa ana maslahi binafsi ya kesi hiyo, haiwezekani hata Mahakama Kuu idharauliwe kwa kuwa hakuna mtu aliyekuwa juu ya sheria.

Aliongeza kuwa inawezakana hata mtuhumiwa huyo anaweza hata kufa na tayari amekwisha athirika kisaikolojia.

“Tunaomba Rais kuingilia kati suala hilo kwa kuwa vyombo vya dola vinakiuka sheria,” alisema Bi Winnie

Katika hukumu hiyo ambayo mlalamikaji aliiomba Mahakama Kuu kusikiliza shauri hilo kwa hati ya dharula ambapo aliwashtaki Mkuu wa Kituo cha Polisi Osterbay  (OCS), Mkuu wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, (RPC), Mkuu wa Polisi Nchini, (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Katika hukumu hiyo iliyotolewa Oktoba 19 mwaka huu, jaji Ndyansobera aliamuru mtuhumiwa  Zakaria Antony Kapama achiwe huru kwa kuwa aliwekwa mahabusu muda mrefu tangu alipokamatwa Oktoba 10 mwaka huu bila kuwepo na misingi ya kisheria, lakini mpaka tuchapisha habari hizi alikuwa bado yuko mahabusu.

Katika hukumu hiyo ,  jaji Ndynsobera alisema baada ya kusikiliza shauri hilo aliona kuwa misingi ya kisheria kumweka ndani mtuhumiwa hiyo hazikufuatwa na kuangiza polisi kumwachia huru na kuwataka kuhakikisha wanafuata sheria kabla ya kumweka mtuhumiwa mahabusu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *