Click here

Na Mwandishi Wetu

Polisi wa Kituo cha Osterbay jijini Dar es Salaam, katika hali ya kushangaza wamegoma kutekeleza amri ya Mahakama Kuu kumwachia mtuhumiwa aliyewekwa mahabusu muda mrefu kinyume na sheria.

Kwa mujibu wa hukumu ambayo shauri lilifunguliwa kwa hati ya dharula,  Mahakama Kuu mbele ya jaji W.P Ndyansobera Oktoba 19, mwaka huu, polisi waliamuriwa kumwachia mtuhumiwa aliyekamatwa katika Kituo cha Polisi Oster bay na kuwekwa mahabusu kinyume na sheria .

Katika hukumu hiyo ambayo mlalamikaji aliiomba Mahakama Kuu kusikiliza shauri hilo kwa hati ya dharula ambapo aliwashtaki Mkuu wa Kituo cha Polisi Osterbay  (OCS), Mkuu wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, (RPC), Mkuu wa Polisi Nchini, (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Katika hukumu hiyo iliyotolewa Oktoba 19 mwaka huu, jaji Ndyansobera aliamuru mtuhumiwa  Zakaria Antony Kapama achiwe huru kwa kuwa aliwekwa mahabusu muda mrefu tangu alipokamatwa Oktoba 10 mwaka huu bila kuwepo na misingi ya kisheria, lakini mpaka tuchapisha habari hizi alikuwa bado yuko mahabusu.

Katika hukumu hiyo ,  jaji Ndynsobera alisema baada ya kusikiliza shauri hilo aliona kuwa misingi ya kisheria kumweka ndani mtuhumiwa hiyo hazikufuatwa na kuangiza polisi kumwachia huru na kuwataka kuhakikisha wanafuata sheria kabla ya kumweka mtuhumiwa mahabusu.

Akizungumza na Morningstar Post, Oktoba 21 mwaka huu kwa njia ya simu majira ya saa nane mchana, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Jumanne Mlilo alisema kuwa hana taarifa na   hukumu hiyo.

Alisema kuwa katika utendaji wa serikali mifumo ya utendaji inashabihiana, hivyo alimtaka mwandishi kumpelekea nakala ya hiyo ya hukumu ingawa alikataa kurushiwa kwa njia ya mtandao.

Msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime alipopigiwa simu kuulizwa polisi kupinga amri hii ya Mahakama Mkuu kwa kituo cha polisi Osterbay hakuweza kusema lolote.

Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Profesa Ibrahim Juma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *