Na Mwandishi Wetu,

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, Bw. Ombeni Nanyaro, ametoa msaada wa dawa ya kuangamiza mchwa wanashambulia majengo ya shule ya sekondari Msangano, wilaya Momba mkoa Songwe,

Bw. Nanyaro, ambaye amekuwa mdau wa maendeleo katika wilaya Momba mkoa Songwe ametoa msaada wa dawa ya kuangamiza mchwa baada ya kuona kuwa ni tatizo sugu katika majengo ya shule hiyo.

Katika mahafali ya shule hiyo yaliofanyika hivi karibuni  Bw. Nanyaro alitoa msaada wa mchango wa ujenzi wa mabweni ya wasichana wa shule hiyo kiasi cha shilingi 2,000,000 na kuahidi kompyuta, luninga  na mchango wa mafuta ya kuendesha mradi wa maji katika shule hiyo ambao hakuna umeme mpaka pale umeme utakapopatikana.

Akizungumza na Morningstar Post , Bw Nanyaro alisema kuwa dawa hizo zitasaidia kukomesha tatizo la mchwa ambao wanakula mbao za majengo ya shule.

Bw. Nanyaro amekuwa mstari wa mbele katika kusaidia shughuli za maendeleo mkoa wa Songwe kwani hivi karibuni alichangia ujenzi wa mradi wa daraja wilaya Momba ambako ilikuwa ni changamoto kubwa kwa watumiaji.

 

Mjumbe wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Bw. Ombeni Nanyaro akizungumza na mwandishi wa Morningstar Post ofisini kwake kuhusu dawa ya kuua mchwa aliyotoa msaada kwenye shule ya sekondari Songwe wilaya ya Momba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *