Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, mkoa wa Songwe Bw. Ombeni Nanyaro akizungumza kwenye mahafali ya shule ya Sekondari ya Msangano wilaya ya Momba mkoa wa Songwe.

Na Mwandishi Wetu, Momba

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, Bw. Ombei Nanyaro, amewataka wazazi na walezi kuendelea kusomesha watoto wa kike kwa kuwa ni msaada zaidi kwa taifa na wazazi.

Akizungumza akiwa mgeni  rasmi katika mahafali ya shule ya sekondari Msangano, wilaya Momba mkoa Songwe, Bw. Nanyaro, alisema watoto wa kike wakisomeshwa vizuri wanauwezo mkubwa wa kusaidia familia na wazazi wao kuliko watoto wa kiume.

“Mtoto wa kike anauwezo wa kumsaidia mzazi wake zaidi, watoto wa kike hawashikwi, lakini sisi watoto wa kiume tunashikwa, tukishikwa hatuwezi kusaidia wazazi” alisema Nanyaro.

Aidha, Bw Nanyaro aliwataka walimu na madaktari waheshimiwe katika jamii zetu kwa kuwa hao ndio wazalendo wa kweli kwa kuwa asili ya kazi zao hazina uchakachuaji (ubabaishaji).

Alisema wazazi wanawapeleka watoto wao shuleni, wazazi wanaakiri na fedha nyingi lakini wanategemea walimu kufundisha watoto wao na walimu wanafundisha bila kuchakachua.

Aliendelea kusema kuwataka walimu na madaktari waungwe mkono kwa kuwa kazi zao haziwezi kuchakachua.

Katika mahafali hayo Bw. Nanyaro alitoa msaada wa mchango wa ujenzi wa mabweni ya waschana wa shule hiyo kiasi cha shilingi 2,000,000 na kuahidi kompyuta, luninga  na mchango wa mafuta ya kuendesha mradi wa maji katika shule hiyo ambao hakuna umeme mpaka pale umeme utakapopatikana.

Akizungumza katika mahafali hayo mkuu wa shule hiyo, Athans Ernest Mwasoni, alishukuru michango hiyo na kuwataka wadau wengine kujitokeza kusaidia taasisi za elimu.

Alisema kuwa shule hiyo ilikuwa inakabiliwa na changamoto ya mabweni ya wasichana ambayo yalikuwa yamechakaa sana.

Bw. Nanyaro amekuwa mstari wa mbele katika kusaidia shughuli za maendeleo mkoa wa Songwe kwani hivi karibuni alichangia ujenzi wa mradi wa daraja wilaya Momba ambako ilikuwa ni changamoto kubwa kwa watumiaji.

Mradi wa maji wa shule ya sekondari ya Msangano

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *