Na Waandishi Wetu

Mfanyakazi wa Kampuni ya Yapi Markez, Mhandisi Vakkas Cevik, ametoroshwa nchini baada ya kushtakiwa kwa kujihusisha na mapenzi ya wanawake zaidi ya mmoja na kusambaza picha za ngono za wanawake.

Mfanyakazi huyo raia wa Uturuki, alikamatwa na polisi Kituo cha Polisi Salender Bridge na kufunguliwa mashtaka namba SLB/RB/257/23 kwa matumizi mabaya ya mtandao.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa Morningstar Post, mfanyakazi huyo alihusika kufanya mapenzi ya wanawake zaidi ya mmoja (group sex) na kupiga picha za ngono ambazo Morningstar POST ilifanikiwa kuziona picha hizo.

Mfanyakazi huyo baada ya kupiga picha za ngono kwa kutumia simu yake ya mkononi aliwaonesha baadhi ya watu  na kuzisambaza kwa wafanyakazi wengine wa Africa Princess Casino iliyoko maeneo ya Posta jijini Dar es Salaam.

Hatua hiyo ya Mturuki huyo kusambaza picha za ngono za wanawake huku akijitapa kwa wafanyakazi wa casino hiyo ilipelekea mmoja wa wafanyakazi wa casino hiyo kufungua mashtaka polisi na Mturuki huyo kukamatwa na kupewa dhamana.

Polisi wa kituo cha Salender  Bridge walikamata simu za mtuhumiwa na baadhi ya wafanyakazi waliotumiwa picha hizo na kufanya upelelezi lakini wafanyakazi wengine mpaka leo hawajarejeshewa simu zao na Mturuki alipewa simu yake kutoroshwa nchini.

Walalamikaaji waliofanyiwa vitendo hivyo vya unyanyasaji wa ngono walisema kuwa polisi wa kituo cha kati (Central) wamekalia kesi hiyo bila kuchukua hatua za kisheria mpaka mtuhumiwa huyo ametoroshwa nchini.

“Polisi wanasema kuwa faili limepelekwa kwa mwanasheria wa serikali kwa zaidi ya miezi sasa hakuna kinachoendelea”, walisema.

Akizungumza na Morningstar Post, Afisa Usalama wa Yapi Markezi alifahamika kwa jina la moja la Masawe, alisema mfanyakazi huyo hayupo nchini baada ya kumaliza majukumu yake ya kazi.

Akizungumzia suala hilo la unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake, Masawe alimtetea Mturuki huyo kuwa yeye na wanawake hao walikuwa katika mahusiano yao ya mapenzi, uongozi wa Yapi Markez hauwezi kuingilia suala hilo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Debora Magiligimba, alipotafutwa kwa zaidi ya siku tano na waandishi wa habari hizi kwa njia ya simu alishindwa kutoa maelezo yoyote licha ya kuonesha kufahamu vizuri suala hilo.

Katika hatua nyingine

Dada anayedaiwa kufanyiwa vitendo vya unyanyasaji wa kigono na Mturuki huyo Vekkas ameendelea kupata masahibu makubwa kazini kwake baada ya meneja wake aliyefahamika kwa jina la Ergun ambaye anamahusiano ya ujamaa na Vekkas kumshutumu kwa nini alifumngulia kesi Mturuki mwenzake.

Meneja huyo wa Africa Princess Casino, Bw Ergun alimshutumu dada huyo na kuamua kumwahamisha nafasi yake ya kazi kutoka mapokezi na kumpeleka kuosha vyombo jikoni nafasi ambayo alishindwa kuendelea nayo na  kuamua kuacha kazi bila kupenda kinyume na taratibu na sheria zinazosimamia michezo ya kubahatisha.

Kwa mujibu wa sheria zinazosimamia michezo ya kubahatisha wafanyakazi wote wanaoajiriwa kwenye Casino wanapaswa kusajiliwa na nafasi zao za kazi kuanishwa wazi na Bodi ya Michezo ya kubahatisha na kupewa vitambulisho kutoka kwenye bodi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari hizi, Kaimu Mkurugenzi wa Bodi hiyo, Bw. Daniel Ole Sumayan alisema kuwa bodi haiwezi kufumbia macho vitendo vya unyanyasaji wa aina yoyote katika maeneo ya michezo ya kuhabatisha.

Alisema kuwa kwa mujibu wa sheria wanaoendesha michezo ya kubahatisha wanapaswa kuwa ni watu safi na biashara inayotakiwa kufanyika katika sehemu hizo ni michezo ya kubahatisha tu na sio vinginevyo.

Aidha, mkurugenzi huyo ameahidi kushughulikia suala hilo kikamilifu. Na Morningstar Post inaendelea kufanya uchunguzi zadi kuhusu suala hilo.


Mhandisi Vekkas Cevik anayedaiwa kufanya mapenzi ya wanawake zaidi ya mmoja na kusambaza picha za ngono hadharani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *