Na. BBC
Meli ya mafuta ya Urusi iliyokuwa na wafanyakazi 11 imegongwa katika shambulio la Ukraine katika Bahari Nyeusi, maafisa wa Urusi wanasema.
Walisema chumba cha injini ya meli hiyo kiliharibika katika shambulio hilo la usiku kucha katika Mlango wa Kerch. Hakuna aliyeumia.
Ukraine haijatoatamko lolote. Lakini chanzo cha usalama cha Ukraine kiliiambia BBC kuwa boti isiyo na muelekezaji ilitumiwa.
Tukio hilo ni la pili katika siku kadhaa za mashambulizi yanahusisha silaha hizo. Urusi, hata hivyo, haijakiri kuwa uharibifu wowote ulitokea wakati wa shambulio la Ijumaa.
Boti zisizo na nahodha, au droni za baharini, ni boti ndogo zisizo na muelekezaji zinavyofanya kazi juu au chini ya maji.
Utafiti wa BBC unaonyesha – Ukraine imefanya takribani mashambulizi 10 kwa kutumia meli zisizo na nahodha – zikilenga meli za kijeshi, kituo cha jeshi cha wanamaji wa Urusi huko Sevastopol, na bandari ya Novorossiysk. Kwa kuzingatia taarifa za mamlaka ya Urusi na Ukraine, na ripoti za vyombo vya habari vya ndani.
Kerch Strait inaunganisha Bahari Nyeusi na Bahari ya Azov, ikitenganisha Crimea – rasi ya Ukraine iliyochukuliwa na Moscow mwaka 2014 – na rasi ya Taman ya Urusi.
Kulingana na huduma ya usalama ya Ukraine SBU, operesheni ya Jumamosi pia iliendeshwa kwa pamoja na jeshi la wanamaji la Ukraine na kwamba kilo 450 za vilipuzi vya TNT vilitumika.
