Na Mwandishi Wetu

Kigogo mmoja anayefanya kazi Chuo cha Kodi kilichopo Mikocheni jijini Dar es Salaam, ambaye pia alikuwa mgombea wa nafasi ya NEC kupitia wazazi Ubungo,  Joseph Masatu Chikongoye , anadaiwa kukiuka sheria za ujenzi na ukwepaji wa kodi.

Taarifa za uchunguzi zinadai kigogo huyo kwa kushirikiana na injinia wake amekiuka kwa kushindwa kufuata taratibu za ujenzi.

Inadaiwa kuwa mradi wa jengo la biashara umejengwa na kusimamiwa na injinia anayefahamika kwa jina la John ambaye hatambuliki kwenye Bodi ya Wahandisi (ERB),  na sio mfanyakazi wa kampuni ya ujenzi.

Pia, inadaiwa kuwa malipo ya ununuzi wa vifaa na malipo ya kazi katika mradi huo yamekuwa yakilipwa mkononi bila kupitia akaunti za kampuni zinazofanya ujenzi ili kuwezesha kulipa kodi za serikali, 

Inadaiwa kuwa mradi wa ujenzi huo una thamani ya milioni 542, na bango la mradi (sign board) iliyoko kwenye mradi inaonesha kuwa mkandarasi anayesimamia mradi huo ni kampuni ya ZIONANE CONTRACTORS & GENERAL SUPPLIES COMPANY LIMITED ambayo ni daraja la 5, uwezo wake wa ukomo wa kufanya miradi ya ujenzi (class limit) ni milioni 300.

Kwa mujibu wa taarifa inadaiwa kuwa mkurugenzi wa kampuni hiyo ya JAJI CONSULT CO. LTD ambayo bw Chingoye anahusishwa  kwa kutumia nafasi yake ya kazi na uwezo wa kifedha, waliweza kununua bango la mradi wa ujenzi huo na kusajili mradi bila kufuata taratibu za ujenzi kwa kushirikiana na maafisa wa Bodi ya Wakandarasi (CRB) wasio waaminifu na kufanikiwa kukwepa kodi na kuendesha mradi wa ujenzi wa mamilioni ya shilingi bila kutumia kampuni za ujenzi.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa Morningstar POST, kigogo huyo, anadaiwa kujenga mradi wa ujenzi wa jengo la biashara la ghorofa mbili, maeneo ya Mbezi Kwa Yusufu la zaidi ya thamani ya milioni 500 bila kutumia wakandarasi.

Kwa mujibu wa bango la ujenzi lililowekwa kwenye mradi huyo, Mkandarasi aliyeorodheshwa hana mkataba na kigogo huyo na kampuni yake haina uwezo wa kujenga jengo lenye thamani ya milioni 500 licha ya kuwa limewekwa katika mradi huo kama ndio mkandarasi anayesimamia ujenzi.

Hata hivyo, bango la ujenzi lililopo kwenye mradi huu inadaiwa limeibwa na makampuni yaliorodheshwa kwenye bango hilo hawana mkataba na kigogo huyo.

Hata hivyo tunaendelea kuwatafuta  viongozi wa Bodi ya Wakandarasi (CRB) na Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) kuzungumzia mradi huo na ukiukwaji huo wa sheria unaofanywa na kigogo huyo.

0713685823

Jengo la ghorofa mbili linalodaiwa kujengwa bila kusimamiwa na kampuni ya ujenzi, lakini pia kuikosesha serikali mapato lililoko Mbezi kwa Yusufu Magari Saba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *