Na Mwandishi Wetu

Waendesha pikipiki jijini Dar es Salaam, wamewajia juu mgambo wa jiji hilo kwa kuwakamata mara kwa mara wanapoegesha pikipiki zao mitaani.

Hali ya sitofahamu kwa waendesha pikipiki imezidi kuongezeka kwa kuwepo ongezeko kubwa la mgambo wa jiji na wasio wa jiji wanaokamata pikipiki hizo, mara nyingine wanakuwa wanaambatana na polisi waliovaa sare za kazi.

Wakizungumza na Morningstar POST baadhi ya waendesha pikipiki jijini Dar es Salaam, ambao walikamatwa na mgambo wa jiji, walisema kumekuwa na wizi, uonevu na usumbufu mkubwa kwa waendesha pikipiki katikati ya jiji hilo.

Pia wakati mwingine wamekuwa wakisababisha kutokea kwa ajali kwa kukamata wakati pikipiki zikiwa zinaendeshwa na hakuna askari wa usalama barabarani kwani wanakamata bila kufuata kanuni za usalama barabarani.

Alisema kuwa kauli ya Mkuu wa Mkoa aliyepita Paulo Makonda kuwa pikipiki ziingie katikati ya jiji bado haijateguliwa, wanashangazwa kuona mgambo wanakamata pikipiki hovyo zinapokuwa zimeengeshwa katika mitaa ya katikati ya jiji.

Mmoja wa wamiliki wa pikipiki ambaye hakupenda kujitambulisha alikamatwa mtaa wa Agrey akiwa ameengesha pikipiki yake akinunua mahitaji dukani na pikipiki yake kupelekwa kwenye ofisi za Manispaa ya Ilala (Anatogloe), na kupotezewa muda mwingi bila sababu.

Alisema kuwa wakikamata pikipiki na kuipeleka kwenye ofisi yao wanawatoza Tsh70, 000 kuikomboa, lakini hawapatiwi lisiti. Malipo hayo ni kwa ajili ya faini ya dereva sh20,000 na pikipiki sh50,000.

Afisa Mmoja ambaye alikutwa katika maengesho ya pikipiki ziliokamatwa alijitambulisha kwa jina moja la Frank kuwa pikipiki haziruhusiwi kupaki kwenye maengesho yasiyoruhusiwa.

Akaongeza kuwa mtaa wa Agrey ni mtaa usioruhusiwa kupaki pikipiki, eneo lilotengwa kwa ajili ya kuengesha pikipiki ni katika viwanjwa vya JK kikwete maeneo ya uwanja wa wazi zamani kidonge chekundu.

Akizungumza na Morningstar POST, Naibu Spika wa Bunge wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye ni mbunge wa jimbo la Ilala, Mh. Azan Zungu alisema kuwa suala bodaboda ni changamoto kubwa.

Alisema kuwa amekuwa akisaidia zaidi ya waendesha pikipiki zaidi ya 300 wanaokuwa wanakamatwa hovyo kimakosa na mgambo wa jiji ambao wanadai kuwatoza faidi za kuegeneza pikipiki zao katika maengesho yasio rasmi.

“Mimi wananiletea mashtaka na ninaende kuingilia kati nikigundua wamewakamata ‘kihuni’….. nimeokoa wengi wasilipe faini, kuna baadhi ya wakamataji ni wa ulinzi binafsi ni matapeli wanachukua rushwa kwa wenye pikipiki,” alisema.

Akaongeza kuwa sasa anawatafutia mwarubaini wao kukomesha tabia hii inayolenga kuwachonganisha wananchi na serikali yao.

Mussa Azza Zungu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *