Na Jones Mwangonda
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Ridhiwan Kikwete, amekutana na viongozi wa Taasisi ya Wakorea inayoitwa Kofih Tanzania.
Ridhiwan ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze, lililoko Kibaha mkoa Pwani, amefanya mazungumzo na viongozi wa taasisi hiyo hapa nchini na kufanikisha makubaliano ya kuboresha huduma za afya.
Akizungumzia mkutano huo Ridhiwan, alisema mkutano huo ulilenga masuala mbalimbali ya kuboresha maendeleo hususani huduma za afya hapa nchini.
“Tumekuwa na mkutano mzuri na Taasisi ya Wakorea inayoitwa Kofih Tanzania.Tumekubaliana ushirikiano kwa miaka mitano,”alisema.
Mkutano huo ulilenga kuimarishwa kwa miundo mbinu ya afya hasa hosptali ya wilaya, vituo vya afya na kuwezesha vifaa tiba katika eneo la kina mama na watoto.
Ridhiwan ambaye tangu kushika nafasi ya ubunge wa jimbo la Chalinze, amekuwa akilenga zaidi katika maendeleo ya jimbo hilo katika upande wa afya na miundo mbinu.
Akizungumzia mkutano huo wa taasisi ya Wakorea, alisema umelenga zaidi kuboresha huduma na mahitaji ya vifaa vya huduma za dharura na kuwezesha watendaji wa sekta mafunzo ya ujuzi wa juu katika halmashauri ya Chalinze.
0766 600909
