
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA). imesema mabadiliko ya sheria ya Consumer Installation Facility (Kituo cha Mafuta cha Matumizi Binafsi), imetoa fursa kwa viwanda kufunga vituo hiyo.
Akitoa ufafanuzi kuhusu kiwanda cha kuzalisha chakula cha mifugo, Backbone, kilichopo Kata ya Misugusugu Manispaa ya Kibaha Mkoani Pwani, Mhandisi Joseph shija alisema sheria mpya imewapa sifa kiwanda hicho kupata leseni.
“Hii kampuni tumeipa leseni kwa kuwa wana mashine ambazo haziwezi kufika kwenye vituo vya mafuta” alisema.
Aliongeza kuwa hata kampuni zinazomiliki magari mengi wamenufaika na mabadiliko ya sheria mpya wanaweza kupatiwa leseni hizo .
Awali ewura walikuwa wanakataza wananchi kuweka matenki yenye pampu za mafuta mpaka wamiliki mashamba makubwa ,migodi au taasisi zinazotumia mitambo ambayo haiwezi kufika kwenye vituo vya mafuta lakini sheria hiyo iliwakataa wasafirishaji na wenye viwanda
Mhadisi Shija ametoa ufafanuzi huo baada ya kuchapishwa kwa taarifa na tovuti hii kuwa kiwanda cha Backbone kimekubwa na kashfa ya kuweka matenki ya kituo cha mafuta na kutiririsha maji machafu kwenye mifereji ya maji ya mvua barabarani bila kufuata taaratibu na sheria za nchi.