Ngozi ndiyo kiungo kikubwa zaidi katika mwili wa binadamu na inapaswa kudumu nasi maisha yetu yote. Mbali na kutusaidia kuonekana vijana, kuitunza ngozi vizuri pia kuna manufaa kwa afya yetu kwa ujumla.

Hata hivyo, kwa kuwa ngozi ndiyo kinga inayotenganisha miili yetu na mazingira ya nje, hukabiliwa na mambo mbalimbali yanayoweza kuisababisha kuharibika. Mambo mengi ya kimazingira huchangia kuzeeka kwa ngozi, yakiwemo uchafuzi wa hewa, ozoni na mabadiliko ya tabianchi, anasema Jean Krutmann, profesa wa magonjwa ya ngozi katika Taasisi ya Leibniz ya Utafiti wa Tiba ya Mazingira.

“Kwa miongo kadhaa tuliamini kuwa mionzi ya urujuanimno (UV) ndiyo sababu kuu ya kuzeeka kwa ngozi kunakosababishwa na mazingira, lakini sasa tunajua kuwa hilo si sahihi,” anasema Krutmann.

Mionzi ya UV ni aina ya nishati inayotoka kwenye jua.

“Urefu mwingine wa mawimbi ya mwanga wa asili wa jua unaweza kuchangia kuzeeka kwa ngozi, kwa mfano mwanga unaoonekana kwa macho na mionzi ya infrared.” Anasema hata ongezeko la joto linaweza kuchangia mchakato huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *