NA MWANDISHI WETU
Inspekta wa Jeshi la Polisi Nchini Kata ya Buguruni, ametangaza kupambana na wauzaji wa madawa ya kulevya nchini.
Inspekta Hadinani alitoa kauli hiyo ya kutangaza vita dhidi ya wauzaji wa madawa ya kulevya alipotembelea vijana wanaotumia madawa ya kulevya Kata ya Buguruni kutoa elimu ya ushirikishwaji wa jamii kwenye ulinzi shirikishi katika maeneo yao,
“Mnamo tarehe 19/09/2024 majira ya saa 12:00 huko Mtaa wa Madenge Kata ya Buguruni A/INSP HADINANI alitembelea waathirika wa madawa ya kulevya mateja na kuwapa elimu Waathirika wa madawa ya kulevya na ambao bado hawajaweza kujaribu kutumia madawa hayo.” anasema taarifa kutoka kata Buguruni
Inspekta Hadinani aliwaeleza mateja waweze kuepuka utumiaji wa madawa ya kulevya kwani huua uchumi wa nchi Kwa mtu mmoja mmoja na Taifa Kwa ujumla.
“Ukishatumia madawa ya kulevya huwezi kuwa na nguvu na mawazo ya kufikiria uchumi wako ndio maana hata walioathirika na madawa wako radhi waibe vifaa vya nyumbani mwao na kwenda kuuza Ili mradi wapate madawa hayo” alisema.
Akaongeza kuwa unavyojiingiza Kwenye uraibu huu huwezi hata kushiriki ulinzi jirani kwani wewe mwenyewe ndio mwizi namba moja na hatimaye mnaranda randa mitaani na kuitwa mateja
Aliwaomba wajitahidi waache tabia hiyo sio nzuri na wajitahidi kutumia Methadone Ili kuachana na jambo Hilo.
Aliomba atajiwe wauzaji kadhaa wanaowaletea madawa hayo Ili yeye apambane nao.
Mateja hao walishukuru ujio wa Inspekta Hadinani wa kuwatembelea na kuahidi kuacha uraibu huo haraka iwezekanavyo.
Inspekta Hadinani amekuwa akitembelea makundi mbalimbali katika kata ya Buguruni kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa ulinzi shirikishi katika maeneo yao.