NA MWANDISHI WETU
_Kama unatamani kuanza kufanya biashara mtandaoni, unatamani kuuza bidhaa mtandaoni na kukuza biashara yako, unatakiwa kufahamu siri hii_
Biashara yenye mafanikio ni ile inayotatua changamoto za watu kama biashaara haileti utatuzi wa matatizo ya watu haiwezi kuwa ya uhakika na itakufa kwa kukosa wateja.
Biashara inajengwa na nguzo tatu mteja, bidhaa na suluhisho la changamoto ya mlengwa, kama mambo hayo matatu hayapatikani hakuna muamala wa mauzo unaweza kufanyika.
Kuna msemo wa mjasiliamali maarufu duniani Brian Trace anasema lengo la mjasiliamali sio kutengeneza pesa, lengo la mjasiliamali ni kutatua matatizo ya mlengwa wake, pesa inafuata baada ya hapo.
Kama unafikiri kuanza kuuza bidhaa mtandaoni fikiri soko, kisha usitumie ubongo wako kufikiri biashara gani inalipa ingia sokoni chunguza kuna changamoto gani kwa watu kisha tafuta suluhisho la changamo hiyo kwa bidhaa au huduma.
*Kabla ya kuanza kufanya bishara mtandaoni*
Kabla ya kuamua kurusha tagazo lako kwenye mitandao ya kijamii, hatua ya kwanza unatakiwa kuzingati ni soko utakalolihudumia.
Mtandaoni kuna ushindani mkubwa, kuna kila aina ya matangazo, kila aina ya kelele, kila mmoja anatangaza bidhaa au huduma yake.
Ukishindwa kujitofautisha na washindani, ukishindwa kulenga kundi dogo la watu (target audience), mchakato wa mauzo utakuwa mgumu sana.
Ili kushinda kwenye mauzo unatakiwa kufanya kitu tunaita _specialization_, uchaguzi wa soko lengwa kwenye sekta unayoihudumia.
Mfano kama unauza viatu hilo ni soko pana unatakiwa kujikita kwenye aina fulani ya soko la viatu ili kuua ushindani.
Lakini pia unatakiwa kufanya kitu kigine tunaita _segmentation_, kujikita katika soko lenye kulipa, pia _differentiation_ kujitofautisha na wengine, kujiweka mbali na ushindani.
Leo ntakueleza jinsi ya kuchagua soko lengwa lenye kulipa, kuchagua walengwa wako sahihi wenye matatizo sugu yanayosumbua ili uweze kufanya mauzo kwa urahisi.
*Nini maana ya soko lengwa?* (_target martket_)*
*Target market ni nini?* Hili ni kundi fulani la watu wenye mahitaji yanayofanana, mfano upande wa afya na urembo, hili ni eneo pana sana katika soko, saloon ya urembo inaweza kutoa huduma za aina mbalimbali.
Kama vile kukata kucha, kufanya make up, massage nk. Kwa mfano tukichukua moja katika ya huduma hizo za saloon kama kufanya massage.
Hiyo ndio linakuwa target market yetu au kwa jina lingine ndio _niche_ yetu tunaweza kuongeza zaidi kujipambanua kwa kutoa massage kwa wanaume.
Hilo ni kundi la watu ulilolipambanua vizuri unaweza kufikiri kwa nini tunajiweka kizuizi kwenye soko kwa sababu fedha zetu za kufanya marketing hazitoshi kama utalenga soko pana zaidi ujumbe wa kuwafikishia walengwa wako utakuwa dhaifu.
Pia lengo la matangazo yako ni kwa walengwa wako (prospects), ili kuona tangazo lako na kusema “waoo hili ni kwa ajili yangu”
Hii ndio maana unahitaji kuchagua soko lako lengwa kwa kuwa kila kitu kwa kila mtu inapelekea suala zima la marketing kushindwa kufanya kazi.
Hii haimaanishi huwezi kutoa huduma kwa wengine, elewa kuwa tunajiainisha na huduma lengwa kwa ajili ya kufanya kampeni katika marketing iwe rahisi.
Kujaribu kumlenga kila mtu inamaanisha kuwa haujamlenga mtu yeyote, kwa kuwa na soko pana unaua namna ya kujitofautisha na washindani wako na hivyo kuua kabisa mkakati wa masoko na kuuza inakuwa ni ngumu.
*Jinsi ya kuchagua walengwa wako?*
Baada ya kuelewa umuhimu wa kuchagua target market kabla ya kurusha matangazo yako kwenye mitandao ya kijamii, sasa ni wakati wa kuchagua soko lako lengwa, ebu tuangalie mfano wa mpiga picha anavyoweza kuchagua soko lake lengwa.
Mpiga picha anaweza kuwa anatoa huduma za kupiga picha za harusi, picha za makampuni, picha za waandishi wa habari, picha za familia, hii ni aina pana sana ya soko la picha. Njia nzuri ya kufikiria jinsi ya kuchagua soko lako lengwa ni kutumia kanuni ya PVP Index.
*PVP index* ni ( Personal fulfillment, Value to the marketplace and Profitablility), yaani katika kanuni hii unaangalia Kulidhika kwako wewe binafsi kwa kutoa huduma hiyo kwa kundi la watu fulani, kuna watu huwa wanafanya kazi wasizozipenda kwa sababu ya fedha.
*Personal fulfillment* unaangalia kiwango cha kulidhishwa kwako kutoa huduma hiyo, kiasi gani unafurahi kushughulika na hao watu.
*Value to the marketplace*, unafanya tathimini ya huduma hiyo unayotoa kwenye soko hilo kwa kiasi gani soko hilo linathamini kazi yako.
*Profitability* unaangalia kiwango cha faida kwa kutoa huduma hiyo kwenye soko kinalidhisha ni chenye faida.
Kwa mfano mpiga picha anaweza kuchagua soko lake lengwa kama ifuatavyo:
Kwa kutoa huduma ya kupiga picha za harusi *Personal fulfillment* akajipa alama 5, Value akajipa alama 7, kwenye profitability akajipa alama 9 jumla ya alama 21.
Kwenye kutoa huduma ya picha za makampuni Personal fulfillment akajipa alama 3, value akajipa alama 6, profitability akajipa alama 9 jumla ya alama 18.
Kwenye kutoa huduma ya picha za waandishi wa habari Personal fulfillment akajipa alama 9, value alama 7, profitability alama 2 jumla ya alama 18.
Kwa kutoa huduma ya picha za familia Personal fulfillment akajipa alama 9 value akajipa alama 8 na profitabilty akajipa alama 9 jumla ya alama 26.
Hapa walengwa wa mpiga picha huyu ni wale wanaohitaji picha za familia kwa sababu ndio kazi anayoifurahia yenye faida na inathamani kubwa kwenye soko kuliko zingine.
Hii haimaanishi kuwa huwezi kushughulikia soko lingine bali juhudi zetu za kufanya masoko zitajikita kwenye soko letu lengwa zaidi.
Punde tutakapo dhibiti soko hili ndio tunahama kwenda kwenye soko lingine hivi ndiyo unaweza kuchangua soko lengwa na kufanikiwa katika kufanya mauzo mtandaoni makala ijayo ntakueleza jinsi ya kuandika ujumbe wenye mvuto kwa walengwa wako.
nicheki inbox.
Whatsapp 0765868582