NA MWANDISHI WETU
Gari la Mradi wa Serikali lenye usajili wa namba DFPA, limekutwa likiwa limebeba mizigo ya spea za magari za binafsi kwenye duka la Sino Truck Auto Parts linalomilikiwa na raia wa China.
Morningstar Post, ilifanikiwa kulipiga picha gari hilo lililokuwa limebeba mizigo ya spea za magari kutoka Vingunguti kuelelekea maeeno ya Sokota Temeke jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa raia wa China aliyekutwa katika duka hilo aliyefahamika kwa jina la Yan liwei alikiri kuwa gari hilo ni la mradi ya serikali, lakini wanaofanya hivyo ni marafiki zake wanamsaidia tu.
Magari yanayosajiliwa kwa namba za DFPA ni magari ya miradi ya serikali inayopata misamaha ya kodi na husajiliwa na wizara ya Ujenzi.
Morningstar Post inaendelea kufuatilia gari hili kujua zaidi linafanya miradi gani ya serikali.