Benki ya Azani iliyoko barabara ya Nyerere ambayo mbele ya benki hiyyo kuna maji taka yanatiririka barabarani
Sehemu ya mbele ya jengo la Kampuni ya Kamaka ambayo imewapangisha benki ya Azania inaonekana kuritirisha maji machafu barabarani
NA MWANDISHI WETU
Jengo la Kampuni ya Kamaka lililoko barabara ya Nyerere linatiririsha maji taka barabarani.
Kwa mujibu wa habari za ndani inadaiwa kuwa jengo hilo limeunganisha mfumo wa maji taka kwenye mfumo wa maji ya mvua barabarani na hivyo kusababisha maji taka kutapakaa hovyo barabarani.
Meneja wa Benki ya Azania tawi hilo ambaye hakutaka kujitambulisha jina lake alisema kuwa jengo hilo ni la Kamaka na wao hawahusiki na hawajui lolote kuhusu hali hiyo.
Morningstar POST inaendelea kuwatafuta viongozi wa Kamaka kuzunumzia hali hiyo pamoja na watu DAWASA.