Jinsi ya kutangaza facebook au instagram kwa dola moja na kupata matokeo mazuri, usitangaze bidhaa au huduma
NA MWANDISHI WETU
Baadhi ya watu wamekuwa wakitangaza Facebook na Instagram kwa gharama kubwa na wanashindwa kupata matokeo mazuri.
Katika makala haya nta-share na wewe jinsi ya kutangaza Facebook na Instagram bila kutumia gharama kubwa na kupata matokeo mazuri.
Katika mchakato wa kuuza bidhaa mtandaoni kuna hatua tisa unatakiwa kuzipitia kuweza kufanikiwa katika kufanya mauzo ambazo ni:
1. Kutambua soko lako lengwa (target market)
2. Kupanga ujumbe sahihi kwa soko lako lengwa
3. Kutambua chombo sahihi au mahali sahihi pa kutangaza (social media)
4. Kutengeneza mfumo wa kunasa wateja (leads capturing)
5.Kutengeza mfumo wa kutoa thamani (value) kwa walengwa
6.Kutengeneza mbinu za kufanya mauzo, kumgeuza leads kuwa customer
7.Jinsi ya kutoa uzoefu wenye thamani kwa walengwa
8. Jinsi ya kuongeza thamani na kumfanya mteja wako kuendelea kununua kwako.
9. Jinsi ya kutengeneza ubora na kuongeza kujitangaza kupitia wateja wako.
Hatua hizi ni muhimu sana kuzipitia kama unataka kujenga biashara ya uhakika mtandaoni, hata kama utajikuta unauza bidhaa bila kupitia hatua hizi utakuwa unauza kwa bahati na biashara yako haiwezi kuwa endelevu.
Jinsi ya kutangaza Facebook na Instagram kwa gharama nafuu kwanza tambua soko lako lengwa ni kina nani?
Soko hapa ni kundi la watu wenye changamoto zinazofana mfano watu wenye ugonjwa wa kisukari.
Hili ni kundi la watu wenye changamoto ya ugonjwa wa kisukari, kama utakuwa na suluhisho la changamoto hiyo yenye ubora zaidi utaweza kunasa wateja wengi.
Hatua ya pili kabla ya kutangaza Facebook na Instagram unatakiwa kujua ujumbe gani unaenda kuwafikishia walengwa wako.
Kama walengwa wako ni wagonjwa wa kisukari ukipeleka ujumbe usiowagusa hakuna mtu atakuja kwako, mfano ukitangaza jinsi ya kuondoa changamoto ya ugonjwa wa kisukari kwa vyakula au kwa mazoezi au kwa virutubisho kwa namna yoyote ambayo bidhaa yako inafanya.
Hapo kila mwenye changamoto ya ugonjwa wa kisukari atakuja kwako kujua zaidi hapo utakuwa umemnasa prospect (mlengwa)
Ujumbe ni muhimu sana kwenye kutangaza unaweza kutumia sh2500 sawa na dola moja kutangaza facebook kwa siku ukapata wateja wengi kuliko yule anayetumia dola kumi kwa siku ikiwa ataweka ujumbe usio na mvuto bila kujua mlengwa wake ni nani.
Ebu fikiri tangazo lako uliolipia dola moja sawa sh2500 linaonekana kwa watu 800 kwa siku na mwingine analipia dola tano kwa siku tangazo lake linaonekana kwa watu 2000 kwa siku.
Lakini ujumbe ulioweka kwenye tangazo la watu 800 una nguvu na kila watu 800 wanaona tangazo watu 20 wanakuja kwako, lakini yule aliyeweka dola tano wanaona watu 2000 lakini ujumbe hauna mvuto wanakuja watu watano tu.
Kuna umuhimu mkubwa katika kuzingatia mambo niliyoanisha hapo juu kama unataka kufanikiwa katika kupata wateja wengi mtandaoni kwa gharama nafuu.
Kama utapenda kupata mafunzo haya bofya link hapo chini au tuma ujumbe kwenye namba ya whatsapp kujiunga bure kabisa kufurahia mafunzo
0744499499
Kujiunga bofya link hapo chini bure kabisa 👇🏿
https://chat.whatsapp.com/FFRgYyWqp4EKopIGI5IXg1