Na IBRAHIM KADILO

Fikiria kuwa unaamka asubuhi unachukua zana zako na kwenda porini kuwinda wanyama, kuna siku utarudi na nyama kuna siku utarudi mikono mitupu, kila siku unakuwa na presha huna uhakika utapata nyama au utakosa, kila siku ni mpambano.

Sasa fikiri kama mkulima, unapanda mbegu na unasubiri ziwe tayari kwa mavuno, kuna wakati unaziboresha, unaziangalia kwa makini unamwagia maji ukitarajia mazao pale zinapokuwa tayari kuanza kuvuna.

Katika uzoefu wangu watu wengi wanaofanya biashara mtandoni ni wawindaji na sio wakulima, wanatumia kiwango kikubwa cha muda, fedha na nguvu kubwa kujaribu kutafuta wateja wapya na hawafanyi chochote kukamilisha mauzo haraka iwezekanavyo.

Matangazo yao yanalenga katika ushindani wa bei kujaribu kufanya mauzo kwa kujikita kwenye bei na hivyo kuingia katika vita ya bei na washinda wengine, wanatumia muda mwingi kusaka wateja ambao hawana shauku (interest) ya kile wanachokifanya.

Wafanyabiasha wengi hawayatendei haki malengo yao yalioko nyuma ya mkakati wa masoko, wanaweka majina ya biashara, logo, na kauli mbiu zisizo na maana wakidai wanaongoza kwa ubora kwenye sekta yao, ukiwauliza malengo ya matangazo yao wengi watakwambia ni kuuza bidhaa, kufahamika, hii ni makosa, ni makosa makubwa ni kama vile wanatupa fedha ndani ya shimo la choo.

Katika mfumo wa masoko usio wa moja kwa moja (indirect response marketing) lengo la matangazo yako ni kutafuta wateja wenye shauku (interest) kwa kile unachokifanya kuliko kujaribu kufanya mauzo mara moja kutoka kwenye tangazo lako.

Pale mlengwa wako anapoonesha shauku (interest) unamweka mara moja kwenye kumbukumbu zako (database) ambapo unaweza kujenga thamani kwa kujiweka mbele yao kwa kutengeneza athourity (uhalali) kwa kujenga uhusiano na kujenga kuaminika.

Baada ya kufanya hivi mauzo yanafuata bila kuwa na ushawishi wa aina yoyote, iwapo utafanya hayo kwa usahihi kujenga uaminifu, ni mbinu muhimu sana ya kuelewa kwa nini usijaribu kuwauzia moja kwa moja kutoka kwenye tangazo lako.

Ni kweli baadhi ya watu wakiona tangazo lako wanaweza kupelekea kununua mara moja, lakini wengi wao hawatakuwa tayari kufanya maamuzi ya kununua katika siku ya kwanza walipoona tangazo lako, hata kama wana shauku (interest) ya kile unachofanya.

Kama hukuwaweka kwenye kumbukumbu zako umewapoteza, wanaweza kuwa tayari kununua baada ya mwezi, miezi sita au mwaka, kama tangazo lako ni la mara moja umepoteza fursa kwani nafasi ya kukumbuka tangazo lako baada ya miezi sita ni ndogo sana.

Aina hii ya masoko ni kama vile kupanda mbegu kwenye shamba kuzihudumia vizuri, kumwagilia na kusubiri mavuno.

Hata kama ni kwenye walengwa (target market) ndogo walengwa wote hawawezi kuwa sawa na kutendewa kwa usawa, fedha zaidi unazotumia kwenye walengwa wako unajiweka kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuwafanya kuwa wateja wako.

Kumbuka kama unatumia dola 1000 kwenye tangazo ambalo utawafikia watu 1000 ni sawa umetumia dola moja kwa mlengwa mmoja.

Sasa chukulia katika watu 1000 waliofikiwa na tangazo lako watu 100 ni walengwa wako haswa kwenye bidhaa zako kwa kuwachukulia wote hao sawa unakuwa umepoteza dola 900 kwa walengwa ambao hawana shauku na unachofanya na hujawapa motisha wale 100 waliokuwa na shauku.

Badala ya kuwachukulia wote sawa shughulikia walengwa ambao wenye shauku ya juu ya kile unachofanya, usipoteze muda kufanya marketing kwa walengwa wasiokuwa na shauku na kile unachofanya.

Sasa vipi tunaweza kutofautisha pumba na chuya jibu la swali hili ni kutoa rushwa yenye uhalali, tunawapa honga walengwa ili wajieleze wenyewe kwa mfano mpiga picha anaweza kutoa DVD kuwambia walengwa wake haswa kile wanachoweza kuangalia kwenye picha za harusu na kuonesha baadhi ya kazi zake.

Mfano wa tangazo kwa ajili ya kunasa walengwa haswa kichwa cha habari kinaweza kuwa “DVD ya bure inayonesha makosa saba ya kuepuka unapochagua picha za kwenye siku ya harusi” kila maombi ya DVD hiyo itakuwa ni sawa hongo yenye uhalali muombaji atachukuliwa kuwa ni mlengwa haswa wa kile unachokifanya.

Sasa unatakiwa kuchukua jina lake, anuani yake ambayo inakwenda kwenye kumbukumbu zako database yako au kwa namna nyingine jukwaa lako.

Kumbuka lengo ni kutengeze walengwa epuka majaribu ya kutaka kuwauzia kutoka kwenye tangazo lako katika hatua hii unataka kutegeneza leads waliokuwa na shauku ambao wanania ya kweli na wale wasiokuwa na interest na unachofanya ili uwe na database yenye walengwa haswa wenye shauku ya kweli.

Kwa nini watu wengine wanapata walengwa sahihi, wengine wanahangaika kufanya mauzo mtandaoni unatakiwa, kujenga mfumo, unatakiwa kufikiria hilo kuanzia mwanzo hadi mwisho, tunatakiwa kuelewa mfumo unavyofanya kazi na vyanzo vinavyotakiwa kuendesha mfumo huo.

Kitovu cha miundo mbinu ya masoko ni database yako ya walengwa wako kusimamia kumbukumbu zako za walengwa wako vizuri unahitaji haswa uhusiano wa wateja wako ( Customer Relationship Management CRM)

Mfumo wa uhusiano wako na walengwa wako CRM ni kitovu cha masoko ambacho unatakiwa kukisimamia kama mgodi wa dhahabu walengwa wako wote, wateja wako wote kuishia kwenye mfumo huu, hivi ndivyo mambo yanavyenda mtandaoni

Kama utapenda kujifunza zaidi kuhusu mafunzo haya ya jinsi ya kuuza bidhaa mtandaoni usisite tuma ujumbe kwenye namba ya whatsapp ifuatayo au
Kujiunga bofya link hapo chini bure kabisa 👇🏿

https://chat.whatsapp.com/FFRgYyWqp4EKopIGI5IXg1

0744499499

 

 

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *