Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohammed Mchengerwa

NA WAANDISHI WETU

Barabara ya Dawaka iliyoko kwenye maeneo ya viwanda Chang’ombe jijini Dar es Salaam, imeharibika vibaya na kusababisha kero kubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo.

Waandishi wa habari wa Morningstar Post, wameshuhudia barabara hiyo ina mashimo na makorongo kakubwa, na vumbi ya hali ya juu.

Barabara hiyo ambayo ni mtaa ulio na kiwanda cha magodoro, kiwanda cha maji, kiwanda cha bomba za plastiki, Bandari kavu, kiwanda cha simtank na viwanda vingine vingi,

Kwa mujibu wa wafanyabishara ambao hawakutaka kutaja majina yao, wamesema kuwa wakati wa mvua mtaa huo hauwezi kupitika maji yanajaa mpaka yanaingia kwenye viwanda.

Aidha wafanyabishara hao wameiomba serikali kupitia manispaa husika kukarabati barabara hiyo kwa kuwa imeharibisha na kusababisha kero kubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo.

Walisema wafanyabiashara wa viwanda wanaingizia serikali fedha nyingi zinazotokana na kodi hivyo wanaomba kukarabatiwa barabara hiyo ili kuondoa usumbufu na kurahisisha uzalishaji wa viwanda maeneo hayo.,

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *