Na Mwandishi Wetu

Kiwanda cha maji ya kunywa kilichopo Mtwara, Ndanda Springs Limited kinadaiwa kunyanyasa wafanyakazi wake.

Wakizungumza na Morningstar Post, wafanyakazi wa kiwanda hicho zaidi ya 12 wameachishwa kazi bila kulipwa stahiki zao za kazi.

Wafanyakazi hao ambao walikuwa wakifanya kazi katika kiwanda hicho ni pamoja na John John, Julias Mustafa Nchimbi, Evoda Makumbuli na Bashilu Matola.

Wengine ni Juma Kupenda, Ramadhani Hashimu, Zaharan Kapwepwe, Kasimu Msange na Elly Kagonsi.

Wengine ni Ignas Jonathani, Zamda Majal na Happyness Bonifas.

Kwa mujibu wa wafanyakazi hao kiwanda hicho kiliwaachisha kazi bila kuwalipa mishahara ya miezi 4, fedha za likizo kwa miaka miwili na baadhi walikuwa hawasilishiwi michango yao ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii, NSSF.

“Kiwanda kilikuwa chini ya Mzee Madenge baada ya kuja meneja Mwangini mambo ndipo yalipobadilika. Tumeachishwa kazi bila kulipwa haki zetu,” alisema mmoja wa wafanyakazi hao.

Akijibu tuhuma hizo mmoja wa wakurugenzi wa kiwanda hicho Abdulmalik Madenge, alipopigiwa simu kwa namba yake ya mkononi aliwataka waandishi kuwasiliana na meneja wa kiwanda hicho kwa taarifa zaidi.

Hata hivyo,  meneja wa kiwanda hicho Mwangini Madenge alipopigiwa simu kwa simu yake ya mkononi haikuweza kupokelewa hadi tunachapisha habari hizi.

Morningstar POST inaendelea  kuwatafuta viongozi wa kiwanda hicho na mmlaka zingine zinazohusika kuhusuana na suala hil

Maji ya kunywa yanayozalishwa na kiwanda cha Ndanda Springs Limited Mtwara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *