Na Jones Mwangonda

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Wilaya ya Lushoto jiji la Tanga Bw. Ali Dafa, ameahidi kufanyia kazi suala la mgogoro wa ardhi kati ya wanakijiji na Mtanzania mwenye asili ya Kijerumani Bw. William Paulo Penzel.

Mwenyekiti huyo akizungumza na Morningstar POST alisema kuwa amesikia mgogoro huo wa ardhi kati ya wanakijiji wa kijiji cha Malingo Kata ya Mlindi jimbo la Mlalo, lakini hajafikishiwa suala hilo rasmi.

Hata hivyo ameahidi kushughulikia suala hilo ili kuondoa kero hizo za muda mrefu katika kijiji hicho.

Awali Mbunge wa jimbo la Mlalo Wilaya ya Lushoto, Mh. Rashid Shangazi akiongea kwa njia ya simu alisema kuwa suala la mgogoro huo linashughulikiwa na Mkuu wa Wilaya.

“Suala hilo ni la kisheria na liko kwa mkuu wa wilaya linashughulikiwa mimi siwezi kulizungumzia,” alisema Shangazi.

Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Lushoto, alipotafutwa kwa njia ya simu kupitia simu yake ya mkononi haikuweza kupokelewa hadi tunakwenda mitamboni.

Akizungumza na Morningstar Post, Diwani wa Kata ya Mlindi Jimbo la Mlalo, alisema kuwa nyaraka za ardhi zinazoonesha kuwa Bw. Paulo anastahili kumiliki hekari 100 zipo kwenye ofisi ya wilaya.

Alisema kuwa Bw. Paulo alianza kumiliki eneo hilo hekari 800 zilipunguzwa hadi hekari 500 na baadae kufika heka 350.

Bw. Mngumi alisema kuwa suala hilo atalifuatilia na kutia msukumo kwenye ofisi za wilaya ili kuweza kushughulikiwa ipasavyo kwa kuwa limekuwa suala la muda mrefu.

Akizungumzia mgogoro huu diwani alisema kuwa Bw Paulo ni mtanzania amezaliwa nchini, anawajukuu  hapa  hapa nchini hivyo anastahili kumiliki ardhi.

Alisema kuhusu kumiliki ardhi alisema kuwa alikuwa anamiliki hekari 800 tangu mwaka 1987 na serikali iliingia makubaliano nae na kumpunguzia hadi kufika hekari 100 anazostahili.

Suala hilo kwa sasa hivi liko kwenye ofisi ya wilaya ambapo ilipendekezwa kuwa eneo hilo lipimwe na kupata hesabu kamili ya eneo hilo kwani kwa sasa hakuna nyaraka za kiserikali zinaoonesha kuwa eneo hilo ni hekari ngapi isipokuwa kuna maneno tu yanayozungumzwa, alisema diwani.

Hata hivi wananchi wa kijiji hicho walisema kuwa eneo hilo lilipimwa na watu wa ardhi na anatakiwa kumiliki heka 100 lakini hataki kukabidhi hekari zilizobaki.

Wameomba chama chama cha mapinduzi kuingilia kati sula hilo.

Akiongea kwa niaba ya mwenyekiti wa kijiji cha Mlindi Bw. Abdalah Mshingiti alisema kuwa mgogoro huu ni wa muda mrefu kwa sababu kuna watu wanakwamisha juhudi zinazofanywa na uongozi wa kijiji kurudishiwa eneo lao kwa wakati kwa sababu za manufaa yao binafsi.

0766600909

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Wilaya ya Lushoto jiji la Tanga Bw. Ali Dafa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *