Na Fred Okoth

Mwalimu wa shule ya Msingi Majani ya Chai, jijini Dar es Salaam, Elias Japhet amewatapeli walimu wenzake kiasi cha shilingi 300,000 kila mmoja kwa kuwadanganya kuwa angewapandisha vyeo.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa Morningstar Post, mwalimu huyo alimtapeli walimu mwenzake kwa kushirikiana na afisa aliyeko mkoani alifahamika kwa jina la Nyange.

Miongoni mwa mwalimu aliyetapeliwa ni madam Sankala ambaye alitapeliwa shilingi 300000 baada ya kuzungumza na mwandisi wa habari hizi Japhet alirudisha pesa hizo kiasi cha sh70,000 na bado sh230,000.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Japhet alisema kuwa habari hizo ni kweli na hizo ni biashara zake ambazo amekuwa akifanya na kuahidi kumrudishia aliyemtapeli pesa hizo.

“Ni kweli huwa nafanya biashara hiyo unajua mambo ya mjini lakini ikishakuwa na kelele hivyo namrudishia huyo aliyekulalamikia nipe jina lake,”alisema.

Akijibu tuhuma za kushirikiana na Japhet kutapeli sh300000, Bw Nyange alisema kuwa vyeo vinatolewa na Katibu Tawala na Mkurugenzi wa Halmashauri.

Alisema yeye ni nani atoe vyeo anadhani habari hizi ni stori za vijiweni isipokuwa kama kuna mtu analalamika aeleweshwe ajue ukweli huo.

Bw. Nyange alisema kuwa ukiona mtu anatapeliwa apewe cheo tufahamu kuwa hana sifa za kuwa kiongozi vyeo vya uteuzi havipatikana kwa kutoa pesa bali ni utendaji wa kazi na sifa stahiki.

Hata hivyo, Bw. Nyange alikiri kuwa Japhet ni mdogo wake na huenda anatumia ukaribu huo kuweza kutapeli watu na kuomba muda aweze kufanya kazi suala hilo.

Akizungumza na Morningstar Post, Afisa Elimu wa Manispaa Ilala,  alishangazwa na taarifa hizo kwa kuwa vyeo vya walimu haviwezi kupandishwa na mwalimu.

Hata hivyo aliahidi kufuatilia zaidi suala hilo.

Wanafunzi wa shule ya msingi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *