Na Mwandishi Wetu
Diwani wa Kata ya Keko Mwanga, Jasdeep Singh Bahra, anafanya ujenzi wa ghala la kiwanda cha kutengeza T-shirt bila kuwa na vibali.
Kwa mujibu wa uchunguzi ulifanywa na Morningstar Post, umebaini kuwa diwani huyo amekuwa akiwakingia kifua watu wanaokwenda kinyume na sheria katika kata yake.
Watendaji wa halmashuri ya manispaa temeke walifika kwenye mradi wa ujenzi wa kiwanda hicho hivi karibuni na kukuta ujenzi unaendelea lakini diwani huyo alijitokeza na kuzuia watendaji hao kufanya kazi yao.
Aidha waandishi wa habari hizi pia walifika katika mradi huo na kushuhudia ujenzi unaendelea lakini hakuna vibali vya ujenzi.
Akizungumza na waandishi wa habari kwa njia ya simu diwani huyo alikiri kuwa jengo hilo linalojengwa ni la kwake na amewapangisha wachina wanoendesha kiwanda cha kutengeneza fulana.
Habari zinasema kuwa diwani huyo baada ya kuhojiwa na waandishi wa habari hizi alikwenda kulalamika kwenye ofisi za manispaa ya temeke kuwa waandishi wa habari wamempigia simu wanataka kumchafua kwa kuandia habari zake.
“Habari ujenzi za mradi huo sio za kweli mimi sifanyi ujenzi bale…hata wale wachina tumegombana sana kwanini wanafanya ujenzi bila kunihusisha”, alisema diwani
Morningstar Post inaendelea na uchunguzi zaidi
0713685823
Diwani wa Kata ya Keko Mwanga Jasdeep Singh Bahra [katikati] akiwa na madiwani wenzake kwenye ziara