Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amejumuika na waumini wa dini ya Kiislamu, Pemba katika Sala ya Eid El-Hajj iliyosaliwa leo, tarehe 27 Mei 2026, katika Msikiti wa Ole Kianga, Mkoa wa Kusini Pemba.

Mapema baada ya sala hiyo, Alhaj Dkt. Mwinyi alifika Ikulu Ndogo ya Pagali katika eneo maalum lililoandaliwa kwa ajili ya kuchinja mnyama wa (Udh-hiya), ikiwa ni sehemu ya ibada ya Eid, pamoja na kutoa mkono wa Eid kwa Masheikh wa Mkoa huo, kama ilivyo Sunna katika kusherehekea Sikukuu ya Eid El-Hajj.

Waumini wa dini ya Kiislamu duniani kote wanasherehekea Sikukuu ya Eid El-Adha kufuatia kukamilika kwa Ibada ya Hijja, ambayo ni Nguzo ya Tano ya Uislamu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *