BBC

Marekani na Israel “bila shaka zitapata jibu kali”, kiongozi mkuu wa Iran amesema, kufuatia shambulio la Israel dhidi ya Iran wiki moja iliyopita.

Ayatullah Ali Khamenei ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wanafunzi siku ya Jumamosi kabla ya kuadhimisha mwaka wa 45 tangu kunyakuliwa kwa ubalozi wa Marekani mjini Tehran mwaka 1979.

Tisho hilo linakuja wakati Iran ikitathmini jinsi ya kujibu mashambulizi ya Israel ya mwezi uliopita, ambapo Iran ilisema iliwauwa wanajeshi wanne , wakati iliposema kuwa yalilenga kulipiza kisasi kwa shambulio la kombora la Iran dhidi ya Israel mapema mwezi Oktoba.

Shambulio hilo la Iran lilikuja kujibu mauaji ya viongozi wa Hezbollah na Hamas, makundi yenye silaha yanayoungwa mkono na Iran yanayopigana na Israel – na kamanda mkuu wa Iran.

Khamenei amesema maadui wa Iran, ikiwa ni pamoja na Israel na Marekani, “bila shaka watapata jibu kali kwa kile wanachofanya kwa Iran, watu wa Iran na wapiganaji”.

Kinachojulikana kama “mhimili wa upinzani” wa Iran ni muungano wa makundi yanayoungwa mkono na Tehran ambayo ni pamoja na Hamas huko Gaza, Hezbollah nchini Lebanon, Wahouthi nchini Yemen, na makundi yenye silaha nchini Iraq na Syria. Mengi yametajwa kama mashirika ya kigaidi na baadhi ya mataifa ya Magharibi.

Israel inasemekana kusababisha uharibifu mkubwa kwa ulinzi wa anga na uwezo wa makombora wa Iran katika shambulio lake la tarehe 26 Oktoba, ingawa Iran haijakubali hil

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *